James Orengo asisimua mdahalo mitandaoni baada ya kuzungumza sheng

Muhtasari
  • James Orengo asisimua mdahalo mitandaoni baada ya kuzungumza sheng
Image: Twitter/James Orengo

Wanasiasa wengi wanapozungumza na vijana, huwasilisha ujumbe wao kwa njia ambayo inaweza kukaribishwa zaidi na vijana wengi na hii ni kwa kutumia lugha ya Sheng ambayo inakubaliwa na vijana wengi nchini.

Tunapokaribia uchaguzi mkuu, wanasiasa sasa watawashawishi vijana kupitia lugha ya Sheng ili waweze kuwashawishi kuwapigia kura katika uchaguzi mkuu ujao.

Siku ya Ijumaa seneta James Orengo alipakia picha akiwa na wasanii ambao walimtembelea.

Kigogo huyo alisema kwamba atawaunga wasanii mkono kwani wana jukumu muhimu katika jamii.

Ujumbe wake uliibua mdahalo kati ya wanamitandao huku baadhi yao wakimuuliza kama anajua lugha ya sheng.

Pia baadhi yao walisema kwamba wanatambua siasa zinakaribia ndio maana wasanii wameanza kutambuliwa.

" Mbogi Genje wamemuok na wakanipeleka na rieng'. Wasanii wetu wana jukumu muhimu katika jamii yetu na nitajitahidi daima kuwaunga mkono

Hawa wagenje ni warena. Fisted handFisted hand," Orengo aliandika.

Haya hapa baadhi ya maoni ya wanamitandao na wakenya;

agwanda albert: Siaya govana ni mjamoo...wananauo ngumi mbwegze ni maheadbad,leta bladclot Orengo akupige kidi...forms za gwedhe zabe zikiriet ni keuti

Chris: Always interesting how the youth become all important towards elections

Maranga: Mokoro achinawuo amochonke aende retired, vijana wamuok kwa leadership