'Tusisahau mahali tumetoka,'Mchekeshaji Njugush amwandikia mkewe ujumbe wa kipekee

Muhtasari
  • Mchekeshaji Njugush amwandikia mkewe ujumbe wa kipekee
47693210_555842814827055_1227163874537728343_n
47693210_555842814827055_1227163874537728343_n

Mchekeshaji Blessed Njugush na mkewe Celestine Ndinda ni wana ndoa wenye mfano mwema nchini, na wanandoa ambao hawatafuti kiki kwa ajili ya kazi yao.

Wawili hao walipatana wakiwa chuo kikuu na kisha wakafunga pingu za maisha pamoja, na wamebarikiwa na mtoto mmoja.

Huku Njugush akimwandikia mkewe ujumbe anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa alimkumbusha umbali ambao wametoka.

Kulingana na Njugush mambo mengi ambayo wamefanikiwa kuwa nayo yalikuwa ndoto kwao, katika maisha ya awali.

Pia alimshauri mkewe wasisahau umbali wametoka, wala kusahau ndoto zao.

"Furaha ya 29 @celestinendinda .Asante kwa kuweka ahadi yako daima. Uwe na siku nyingi za kuzaliwa. Daima imekuwa  ndoto ...

Tuliota kuwa na  watoto 2 tulikuwa na ndoto ya kuishi katika chumba cha kulala cha 1 .... Tulikuwa na ndoto ya siku moja kumiliki toaster ya mkate (niliona kwa mara ya  kwanza katika chuo kikuu) tulikuwa tukienda kwenyebarabara ya Nyayo na kuchagua gari ambalo tunataka kumiliki,Tusiache kuota kamwe

 Angalia kile umekuwa dendai ..... Angalia mwenyewe. Sasa wanakuita wewe Mama Tugi lol Yaani Huwa Siamini ... Nini zaidi ni Bado Haijafika Mahali Nilikushow .... bora pamoja.

 kamwe tusisahau ambapo sisi tumetoka.. ndiyo sababu picha hii daima ni bora kwangu. Kwa maelezo zaidi @celestinendinda Kam Hivi Nikushow," Aliandika Njugush.