'Hii ni kiki hamna kitu,'Mashabiki wamwambia kipusa anayedaiwa kuwa mpenzi wake Diamond

Muhtasari
  • Wanamitandao wamshambulia kipusa anayedaiwa kuwa mpenziwe Diamond
Diamond

Kipusa anayedaiwa kuwa mshikaji mpya wa staa wa bongo Diamond Platnumz Fancia anasherehekea siku yake ya kuzaliwa hii leo, huku akifikisha miaka 20.

Inamaanisha bado ana mambo mengi ya kujifunza.staa wa bongo Diamond kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alimpakia Fancia, huku aki densi kibao chake.

Pamoja na kumbukumbu zake za awali za kuwa na wake kadhaa na wa kike, kila mtu alikuwa na hamu ya kujua uhusiano wake na mwanamke aliyepakia kwenye  ukurasa wake wa Instagram.

Baadhi ya mashabiki waliesema na kudai kwamba ni kiki tu hamna mapenzi kati ya wawili hao.

Fancia alipakia picha yake kwenye ukurasa wake wa instagram na kujitakia heri njema siku yake ya kuzaliwa ambapo alimtaja Diamond.

Katika Video zake nyingi kwenye ukurasa wake amepakia akisikiza vibao tofauti vya staa huyo.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;

baby_ake: Hapa nishaona kiki hakuna kitu hapa

poka_touches: Hapa tumepigwaaa😂

heaven_raphael2000: Sawa aahachi papuchi uyo😂

maigemariam: Wifiiiiii ❤️❤️❤️😂😂😂

gecha_media: Jaman ishi miaka mana HUKU ushatuvuluga tuna haha kukufahamu 😂 tupe basi hata caption nyingine

Je wawili hao ni wapenzi au ni kiki tu kama wanavyo dai mashabiki wengi?