Hizi hapa sababu zinazothibitisha kwa nini Akothee haishi maisha ya mtu mwingine

Muhtasari
  • Hizi hapa sababu zinazothibitisha kwa nini Akothee haishi maisha ya mtu mwingine
akoth stylish 1 (1)
akoth stylish 1 (1)

Msanii Akothee ni miononi mwa wasanii na watu mashuhuri ambao, wanaishi maisha yao na huwa na msimamo wao katika maisha yao.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo amenakili kwanini huwa haishi maisha ya mtu mwingine.

"Sijawahi kuwa na shida kwanini watu huwa hawanielewi, lakini nina shida kubwa ya kutojielewa mimi ni nani,mhali niipo na nataka kuwa nani

Sijawahi ishi maisha ya mtu mwingine,mimi si wao na wai si mimi,Wao sio kipimo cha mafanikio yangu

Sina wazo la asili yao,kizazi chao, maisha yao ya sasa na ya baadaye,sijui safari yao mahali inawapeleka 

Sina wazo la kile wanapitia na jinsi na vile maisha yao ya zamani yalikuwa, kwa kifupi kila mtu anapaswa kufanya kazi yake, ni rahisi sana kila mtu kuishi maisha yake

Usimumizwe moyo katika mitandao ya kijamii ya wasanii na watu mashuhuri na vifurushi ya data ambavyo ulinunua na pesa yako

Mpe block na kutomfuata mtu au kitu ambacho hakikutii moyo una uamuzi wako, ni wewe unasoma maisha yako yakiwa chini," Akothee Aliandika.