'Siishi na watu bandia kama wewe,'Zari Hassan ampa msomo rafiki yake mnafiki

Muhtasari
  • Zari Hassan ampa msomo rafiki yake mnafiki
Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Zari Hassan kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amempa msomo rafiki yake aliyemuita kama mnafiki.

Zari anafahamika kwa kuishi maisha ya kifahari na kuwatambu marafiki zake kila wakati, lakini inaonekana kuna mmoja ambaye amemfika kwenye koo kwa unafiki wake.

Kulingana naye amemtishia kufichua siri zake kwani amemsaidia ya kutosha lakini haoni hayo yote.

Pia aliweka wazi kwamba haishi na watu bandia, kwani hapendi drama katika maisha yake, n anapenda kuishi maisha yake bila drama yeyote.

Amefichua kwamba mwanamke daima alitumia faida yake kwa kiasi kikubwa kwa kiwango ambacho alikuwa mwenye furaha wakati Zari alimtambulisha, kwenye mitandao yake ya kijamii.

Hakika hatujui kile mwanamke alichofanyia Zari lakini inaonekana kuwa ni kubwa sana na msichana wetu amesema yametosha kwa sababu yeye hataki chochote cha kufanya naye tena.

"Naishi maishi ya huru kwani sipendi drama, na siishi wala kushinda na watubandia  kama wewe ulikuwa hapa kwa ajili ya mashabiki tu

Ulipopata wafuasi wengi mitandaoni kwa ajili yangu, ulikuwa na uraha kama mtoto mdogo, sababu ya kuachana na wewe ilikuwa zaidi ya masengenyo yako ya kiki kwenye televisheni

Mimi ni mtu wa mwisho ambaye unataka kumuudhi,nitafichua uchi wako,usije kwani labda nikiwa nimekupigia simu

Aliyekuwa mume wako atashangaa kama alikuwa ameoa mahosha au mke,kuja pole pole dada yangu, sifanyi drama Nilichoma jumbe lote siishi hapo, amani," Aliandika Zari.