Mwaka wa baraka! Baadhi ya watu mashuhuri ambao wamebarikiwa au wanatarajia watoto mwaka huu

Muhtasari

•Habari kuhusu ujauzito wa mwanamuziki mashuhuri kutoka Bongo Vanessa Mdee zilisisimua mitandao siku ya Jumanne.

Image: INSTAGRAM

Mwaka wa 2021 umeonekana kuwa wa fanaka kwa wanandoa wengi mashuhuri.

Licha ya kuzorota kwa  sekta ya usanii kutokana na janga la Corona, sio kila upande uliozorota. Baadhi ya wasanii mashuhuri katika ukanda wa Afrika Mashariki wamebarikiwa na watoto katika kipindi hicho huku wengine wakitangaza kuwa wanatarajia kupata hivi karibuni.

Habari za ujauzito wa mwanamuziki mashuhuri kutoka Bongo Vanessa Mdee zilisisimua mitandao siku ya Jumanne.

Vanessa pamoja na mpenzi wake mwigizaji Rotimi walitangaza kuwa wanatajia mtoto wao wa kwanza hivi karibuni.

Wawili hao walipakia picha za ujauzito na kuambatanisha na jumbe za kuonyesha furaha yao kutokana na mafanikio hayo. 

Wasanii hao wamekuwa kwenye uhusiano tangu mwaka wa 2019.

Kando na Vanesaa Mdee na Rotimi, fahamu baadhi ya watu wengine mashuhuri ambao wamebarikiwa na mtoto ama wanatarajia mtoto mwaka huu:-

1. Vera Sidika na Brown Mauzo

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Habari za ujauzito wa mwanasoshalaiti mashuhuri Vera Sidika zilienea sana mitandaoni mwezi Julai baada yake kutangaza hadharani kuwa anatarajia mtoto wake wa kwanza na mpenzi wake mwanamuziki Brown Mauzo.

Mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 31 na anayemezewa mate sana kutokana na unene wa makalio yake alifichua kuwa anatarajia mtoto wa kike kabla ya mwaka huu kuisha.

Mfanyibiashara huyo amekuwa akipakia picha na video za ujauzito wake mitandaoni tangu atangaze habari hizo.

2 Size 8 na DJ Moh

Wiki iliyopita wanandoa mashuhuri Size 8 na DJ Moh walitangaza kuwa wanatarajia mtoto wao wa tatu.

Wawili hao walitumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kufahamisha mashabiki wao kuhusu mafanikio hayo.

Wamekuwa kwa ndoa tangu mwaka wa 2013 na tayari wana watoto wengine wawili; Ladasha na Muraya Juniour.

3. Corazon Kwamboka na Frankie

Frankie, Corazon Kwamboka na mtoto wao
Image: Instagram/Frankie

Hivi karibuni mwanasoshalaiti Corazon Kwamboka na mpenzi wake Frankie Just Gymit walitangazia mashabiki wao kuwa wanatarajia mtoto wao wa pili.

Wawili hao walipakia picha za kufichua ujauzito na kusema  kwa wana furaha kuona familia zao zinapanuka.

Mwaka uliopita wapenzi hao walikaribisha mtoto wao wa kwanza baada ya kuchumbiana kwa kipindi kifupi.

4. Willis Raburu na Ivy Namu

Takriban miezi miwili iliyopita mtangazaji mashuhuri Willis Raburu na mpenzi wake Ivy Namu walimkaribisha duniani mtoto wao wa kwanza.

Raburu alifahamisha mashabiki wake kuhusu mafanikio hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram mwezi Agosti.

Mtumbuizaji huyo amekuwa kwenye mahusiano na Ivy Namu kutoka Uganda kwa muda sasa ingawa wawili hao wamekuwa wakiweka uhusiano wao kisiri.

5 Daddie Marto na Christine Koku

Image: Instagram/Daddie Marto

Mwishoni mwa mwezi Agosti mwigizaji Martin Githinji almaarufu kama Daddie Marto na mpenzi wake Christine Koku Lwanga walikaribisha mtoto wao wa pili.

Wawili hao walifunga ndoa mwaka wa 2018 na tayari wana mtoto mwingine wa kiume.