'Ujauzito sio ulemavu, sikupangia ujauzito wangu wa pili,'Corazon Kwamboka asema

Muhtasari
  • Siku chache zilizopita Corazon Kwamboka na mpenzi wake Frankie walitangaza kuwa wanatarajia mtoto wao wa pili
Frankie, Corazon Kwamboka na mtoto wao
Image: Instagram/Frankie

Siku chache zilizopita Corazon Kwamboka na mpenzi wake Frankie walitangaza kuwa wanatarajia mtoto wao wa pili.

KUpitia kwenye sekta ya Q&A  kwenye mitandao ya kijamii ya instagram Corazon alisema kwamba hakuwa amepangia ujauzito wake wa pili.

Hii ni baada ya mmoja wa mashabiki wake kumuuliza kama alikuwa amepangia ujauzito wake.

Ni habari ambazo ziliwashangaza wengi hasa mashabiki wake, licha ya hayo alisema kwamba alifurahi baada ya kupata kwamba ana ujauzito.

"Je ulipangia mtoto wako wa pili,mimi ni mama kwa mara ya kwanza kupitia upasuaji na nina panga kupata mtoto wa pili," Aliuliza shabiki.

Corazon alijibu;

"Hapana lakini nilifurahi wakati nilifahamu," Alijibu.

Pia alisema kwamba ujauzito sio ulemavu, baada ya shabiki kumuuliza kama kifungua mimba wake kuna kitu anakosa baada ya kupata ana ujauzito.