(Video) Sina Neno! Jux amwandikia wimbo aliyekuwa mpenzi wake Vanessa Mdee kumpongeza kwa ujauzito, asema hana chuki

Muhtasari

•Jux amesema kuwa ana raha sana kuona kwamba Mdee anafurahia ndoa yake ya sasa na mwigizaji Rotimi na kumpongeza kwa kuwa hivi karibuni ataweza kuitwa mama.

•Msanii huyo amesema kuwa hana chuki yoyote na Mdee na kudai kuwa anamwombea maisha ya furaha pamoja na mpenzi wake. Amewashauri wavumiliane na wasiwahi kugombana ili mtoto wao asiwahi pata shida.

Image: INSTAGRAM

Staa wa Bongo Juma Jux ametoa wimbo wa kumpongeza aliyekuwa mpenzi wake Vanessa Mdee baada yake kutangaza kuwa ni mjamzito

Kwenye wimbo 'Sina Neno' ambao alipakia kwenye mtandao wa Youtube siku ya Jumatano, Jux amemhakikishia Mdee kuwa hana ugomvi wowote na yeye kwani alishafunika yaliyopita kwenye kaburi la sahau.

Jux amesema kuwa ana raha sana kuona kwamba Mdee anafurahia ndoa yake ya sasa na mwigizaji Rotimi na kumpongeza kwa kuwa hivi karibuni ataweza kuitwa mama.

"Naona wameremeta, ngozi imenawili una furaha now,

Kitanda hakina siri, zao la tendo una kitumbo wow,

Mnapendeza sana na penzi liko kasi kasi

Mkipostiana, Instagram status..." Jux amesema kwenye wimbo huo.

Msanii huyo amesema kuwa hana chuki yoyote na Mdee na kudai kuwa anamwombea maisha ya furaha pamoja na mpenzi wake. Amewashauri wavumiliane na wasiwahi kugombana ili mtoto wao asiwahi pata shida.

"Najua una furaha kwa zawadi uliyopata.

Tena ulivyo shujaa,mtoto mama amepata. 

Na nyie msije gombana, mtoto asije akapata kash kash 

Uzuri kuvumiliana, matatizo mkadiscuss

Tulishafunika kurasa, mambo ya zamani yalishapita

Maisha mengine sasa, kuwa na amani hakuna vita

Sikuchukii nakuombea,

Maisha mema ya furaha, Mungu awaonyeshe njia

Siumii, nimezoea, ila nina furaha kuiona familia

Niko salama, Mimi sina neno" Jux amesema

Jux releases his fresh new single titled "Sina Neno". This song is dedicated to all his fans. The official audios are now out and available in different platforms. Mapepe and Sawa official audios are out now. KingOfHearts Available Worldwide: http://africori.to/juxthelovealbum.oyd © 2021 African Boy Follow Jux Facebook: https://www.facebook.com/Juma-Jux-553 Instagram: https://www.instagram.com/juma_jux/ Twitter: https://twitter.com/africanboyjux More from Jux: Now You Know ft. Q Chief: https://youtu.be/Y-LhxgM3xS8 Wambela ft. Ruby: https://youtu.be/FsTP1qc9VXA Jux - Sina Neno Lyrics Intro Ayeeeaaa yeee Ayeeeaaa yeee Ayeeeeeee Verse:1 Naona wameremeta Ngozi imenawili, una furaha now Kitanda hakina siri Zao la tendo, una kitumbo wow Mnapendezana Penzi liko kasi kasi Mkipostiana Instagram status Tushafunika kurasa Mambo ya zamani, yalishapita Maisha mengine sasa Kuwa na amani, hakuna vita Pre-Chorus Siiikuchukii nakuombea Maisha mema ya furaha, Mungu aoneshe njia Siiiumiii nimezoea Ila na furaha, kuiona familia (Aaaah aaah) Chorus Niko salama, mimi sina neno. (Aaaah aaah) Utaitwa mama Mtoto mpe upendo (Aaaah aaah) Niko salamaaaa, mimi sina neno. (Aaaah aaah) Utaitwa mama Mtoto mpe upendoo (Aaaah aaah) Uuuuuuuh Iyeeeeee yeee Iyeeeee yeee Iyeeeee yeee Verse:2 Najua unayo furaha Kwa zawadi uliopata Tena ulivyoshujaa Mtoto mama amepata Na nyie msije gombana Mtoto akapata kashi kashi Vizuri kuvumiliana Matatizo mkaya discuss Tushafunika kurasa Mambo ya zamani, yalishapita Maisha mengine sasa Kuwa na amani, hakuna vita Pre-Chorus Siiikuchukii nakuombea Maisha mema ya furaha, Mungu aoneshe njia Siiiumiii nimezoea Ila na furaha, kuiona familia (Aaaah aaah) Chorus Niko salamaaaa, mimi sina neno. (Aaaah aaah) Utaitwa mama Mtoto mpe upendo (Aaaah aaah) Niko salamaaaa, aaaaaah aaah. (Aaaah aaah) Utaitwa mama Mtoto mpe upendoo (Aaaah aaah) #Jux #SinaNeno #KingOfHearts

Jux na Vanessa walitengana mwaka wa 2019 baada ya kuchumbiana kwa kipindi kirefu. Hata hivyo, Vanessa alifichua kuwa wao ni marafiki wakubwa licha ya kuenda njia tofauti.