'Wanawake Kenya wanapenda wanaume wenye maumbile makubwa' Mamitto aeleza sifa wanazoangazia wanawake kwa mwanaume

Muhtasari

•Kulingana na Mammito ikiwa mwanaume hana hela ni heri basi awe na maumbile makubwa ili aweze kutosheleza mpenzi wake kitandani.

Image: INSTAGRAM// MAMMITO

Mchekeshaji maarufu nchini Eunice Mammito amesema kuwa wanawake wa Kenya wanapendelea sana wanaume wenye maumbile makubwa kwenye viungo vyao vya uzazi.

Akiwa kwenye mahojiano katika kituo cha Wasafi Media nchini Tanzania, Mammito alichua kuwa pesa na maumbile makubwa ni baadhi ya sifa ambazo wanawake wengi nchini Kenya huangazia wanapotafuta mchumba.

Kulingana na Mammito ikiwa mwanaume hana hela ni heri basi awe na maumbile makubwa ili aweze kutosheleza mpenzi wake kitandani.

"Tukitoa pesa tunaenda kwa urefu (wa viungo vya uzazi). Tena hutaki uteseke eti mwanaume hana pesa tena urefu..Sidhani kuna mtu anapenda maumbile madogo. Nimekuwa na marafiki wengi sana na wameniambia kuwa pande hizo zikiwa sawa .. unajua kama huna pesa basi heri uwe na maumbile" Mammito alisema.

Mchekeshaji huyo wa Churchill Show pia amedai kwamba kunao baadhi ya wanawake nchini ambao huwalipa wanaume  na kuwatunza vizuri ili wawatosheleze kimapenzi.

"Wapo, wanaitwa wamama wa Harrier. Wana maduka makubwa sana, wanachukua vijana vijana pale wanawaweka kwenye 1 bedroom ama 2 bedroom. Vijana ambao ni watanashati na ambao wana misuli. Wanawaweka pale wanawapea chakula" Alifichua Mammito.

Msanii huyo amekiri kwamba anapenda pesa sana na kusema kuwa maarifa na  uwezo wa mwanaume kifedha ni  baadhi ya sifa ambazo yeye huwa anaangazia kwa mchumba.

"Naangazia hela. Unaona hata mfalme Solomon alikuwa na wanawake wengi lakini alikuwa mfalme mwenye maarifa. Kama huna maarifa basi kuwa na hela. Kwa kweli unaweza kosa hela. Lakini ukikosa hela na ukose maono basi wewe huwezi saidika" Mammito alisema.

Mammito hata hivyo amefichua  kuwa kwa sasa ako kwenye mahusiano na mwanaume ambaye hakufichua na kukiri kuwa hakuna chochote ambacho hawezi kufanya mbele yake ikiwemo kujisaidia.