Mastaa wa Bongo Diamond Platnumz na Harmonize kutumbuiza Marekani mwezi Oktoba

Muhtasari

• Harmonize tayari amefanya tamasha katika jimbo la Ohio na Houston

Image: INSTAGRAM

Siku chache baada ya mwanamuziki Harmonize pamoja na mwenzake Ibraah kuondoka nchini Tanzania kuelekea Marekani kwa ziara ya kimuziki, Diamond Platnumz atakuwa akifanya ziara yake kama ile huko Marekani  mwezi ujao.

Kulingana na tangazo ambalo amechapisha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, Diamond ataanza ziara yake jijini Atlanta, Georgia mnamo Oktoba 8. Siku itakayofuata atafanya tamasha katika jiji la Washington DC.

Mnamo tarehe 15, 16, 17 Oktoba staa huyo wa Bongo atakuwa Minneapolis, Denver na Los Angeles mtawalia.

Tarehe 22, 23 na 24 Diamond atakuwa jijini New York, Louisville na Arizona mtawalia kisha amalizie na Boston, Houston na Dallas mnamo tarehe 29, 30 na 31 mtawalia.

Kwa upande wake Harmonize tayari amefanya tamasha katika jimbo la Ohio na Houston huku akitazamia kutumbuiza mji wa Phoenix na Las Vegas mnamo tarehe 18 na 23-25 mtawalia mwezi huu.

Mwezi wa Oktoba Harmonize atafanya tamasha zingine sita jijini New York, Edmonton(Canada), Los Angeles, Salt Lake, Atlanta na amalizie na  Syracuse, New York mnamo Oktoba 23.