Mwanamuziki Britney Spears 39, atangaza kuchumbiwa na mpenzi wake Sam Asghari mwenye miaka 27

Muhtasari

•Haya yanajiri huku Bi Spears akipambana kisheria kuhakikisha anamaliza miaka yake 13 ya usimamizi wa kisheria wa baba yake mzazi wa mali zake, ambapo kulingana na sheria baba yake ana mamlaka ya kudhibiti maisha yake pamoja na fedha zake.

Image: GETTY IMAGES

Mwanamuziki wa Marekani Britney Spears ametuma video mtandaoni akiwa na mchumba wake na kuonesha pete kwenye mtandao wa Instagram.

Haya yanajiri huku Bi Spears akipambana kisheria kuhakikisha anamaliza miaka yake 13 ya usimamizi wa kisheria wa baba yake mzazi wa mali zake, ambapo kulingana na sheria baba yake ana mamlaka ya kudhibiti maisha yake pamoja na fedha zake.

Alifichua kuwa masharti ya mpango huo yanamzuia kuolewa na Bw Asghari au kuwa na watoto zaidi.

Mpango wa udhibiti wa mali zake uliwekwa mwaka 2008 wakati hofu kuhusu afya ya akili ya muimbaji ilipoibuka.

Bw Asghari alituma picha tofauti ya pete ambapo wapenzi hao walionekana wakibusiana.

Meneja wake, Brandon Cohen, alithibitisha taarifa ya uchumba wao kwa jarida la People.

"Wenzi hao wameufanya uhusiano wao wa muda mrefu rasmi leo na nimeguswa na uungaji mkono uliooneshwa kwao, kujitolea na upendo ulioonyeshwa kwao ," alisema.

Britney na Bw Asghari walikutana walipokuwa wakiandaa video ya muziki katika mwaka 2016.