'Usihukumu,'Bahati asema baada ya mashabiki kumlaani vikali kwa kukejeli Mungu

Muhtasari
  • Bahati azungumza baada ya mashabiki kumlaani vikali kwa kumkejeli Mungu
Bahati kwenye wimbo "Fikra za Bahati'
Bahati kwenye wimbo "Fikra za Bahati'
Image: Instagram

Baada ya msanii Bahati kujipata pabaya mitandaoni baada ya kupakia video inayomuonyesha akijiburudisha na kuiambatanisha na ujumbe ambao wanamitando wengi wamehisi kwamba hauambatani kabisa na anachokifanya kwa video

Kwenye video hiyo ambayo alipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Bahati anaonekana akivuta sigara inayowekwa kwa chupa maarufu kama 'Vape' huku akipiga densi kana kwamba anasherehekea. Kwa wakati huo mwanamuziki huyo ambaye tayari ametangaza kwamba amegura injili anaoekana akiwa amevalia mavazi ya kiarabu.

Chini ya video hiyo Bahati aliambatanisha na ujumbe;

 "Puff' moja to kusherehekea kuwa mwanamuziki bora wa injili na wa ngoma za kutumbuiza kwa mpigo Kenya. Nanyenyekea."

Wanamitandao walidai kwamba msanii huyo alikuwa anakejeli Mungu.

Baada ya msanii huyo kuona hisia za mashabiki, alipakia picha huku akisema kwamba Mungu ni wa kila mtu na wanadamu hawapaswi kuhukumu.

"Usihukumu Mungu wetu sote," Bahati aliandika.

Swali kuu ni je Bahati anaweza kuwa mfano mwema kwa vijana wa sasa au  kwa wasanii chipukizi?