Usiwache wababa hawakusaidii wakupararishe-Huddah Monroe awashauri wanawake

Muhtasari
  • Huddah Monroe awashauri wanawake dhidi ya kuvunja familia za wenyewe
HUddah Monroe
Image: maktaba

Mwanaspsholaiti Huddah Monroe kupitia kwenye ukuraa wakae wa instagrama amewashauri wanawake wasivunje ndoa za wenyewe na wababa amabao hawawezi kuwasaidia maishani.

Hii ni baada ya kuwauliza mashabiki waandike kitu ambacho anaweza kuona ili awajibu kwenye mitandao hiyo.

Baadhi ya mashabiki wake hasa wanawake walifunguka na kusema kwamba waume wao huwa hawawaridhishi kitandani wakati wa tendo la ndoa.

"Usiwache wababa hawakusaidii wakupararishe, ilhali unaharibu na kuvunja ndoa ya wenyewe bure," Huddah Alisema.

Pia kulingana na Huddah ni vyema kuwa na mwanamume ambayeni tajiri na anakusaidia kuliko baba mzee ambaye hakusaidii.

Aidha aliwashauri vijana kuwa makini na ujana wao, kuliko kutumika vibaya au kutumiwa vibaya na wanaume.

Lakini katika karne ya sasa hasa Nairobi, utampata kweli mwanamke ambaye hapendi pesa?