Wanamitandao walaani mwanamuziki Bahati vikali kwa 'kukejeli' Mungu

Baadhi yao walimwambia msanii huyo kwamba angefikwa na mabaya kutokana na ghadhabu ya Mungu.

Muhtasari

•Kwenye video hiyo ambayo amepakia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Bahati anaonekana akivuta sigara inayowekwa kwa chupa maarufu kama 'Vape' huku akipiga densi kana kwamba anasherehekea. Kwa wakati huo mwanamuziki huyo ambaye tayari ametangaza kwamba amegura injili anaoekana akiwa amevalia mavazi ya kiarabu.

Bahati kwenye wimbo "Fikra za Bahati'
Bahati kwenye wimbo "Fikra za Bahati'
Image: Instagram

Mwanamuziki mashuhuri nchini Kelvin Kioko almaarufu kama Bahati amejipata pabaya mitandaoni baada ya kupakia video inayomuonyesha akijiburudisha na kuiambatanisha na ujumbe ambao wanamitando wengi wamehisi kwamba hauambatani kabisa na anachokifanya kwa video

Kwenye video hiyo ambayo amepakia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Bahati anaonekana akivuta sigara inayowekwa kwa chupa maarufu kama 'Vape' huku akipiga densi kana kwamba anasherehekea. Kwa wakati huo mwanamuziki huyo ambaye tayari ametangaza kwamba amegura injili anaoekana akiwa amevalia mavazi ya kiarabu.

Chini ya video hiyo Bahati aliambatanisha na ujumbe "Puff' moja to kusherehekea kuwa mwanamuziki bora wa injili na wa ngoma za kutumbuiza kwa mpigo Kenya. Nanyenyekea."

Chapisho hilo la hivi karibuni halijapokewa vyema na kikundi kikubwa cha wanamitandao huku wengi wakisema kuwa kitendo kile ni cha kukejeli Mungu.

Baadhi yao walimwambia msanii huyo  kwamba angefikwa na mabaya kutokana na ghadhabu ya Mungu.

Hizi hapa baadhi ya jumbe za wanamitandao:-

@hopekidk Unachanganya pia Yesu sasa

@Joyce_mwendo Aki huyu ni Mungu unachezea.. mimi mahali amenitoa siezi aki

@naomy.mu Mungu hapendi mchanganyo.. we hujui unafanya nini. Acha kufurahisha walimwengu

@robbiro20 Utabadilika kuwa nguzo la chumvi.. wewe cheza na Mungu

@dralex_kakai Mungu aki na mpango wako hivi karibuni RIP.. hii ni kejeli

@dkkwenyebeat Nakuombea ndugu