Inavunja moyo!Millicent Omanga ajitolea kumsaidia mwanafunzi aliyeomba msaada wa karo

Muhtasari
  • Millicent Omanga ajitolea kumsaidia mwanafunzi aliyeomba msaada wa karo

Seneta mteule Millicent Omanga ameelezea kusikitishwa baada ya mwanafunzi wa kidato cha pili kuingia barabarani kuomba ada ya shule.

Siku ya Jumatano, Mellan Njeri Njuguna mwenye umri wa miaka 15 aliingia kwenye barabara za Nairobi akiwa na bango, akiomba watu wasamaria wema wamsaidie kupata ada ya shule.

"Tafadhali nisaidie ada ya shule," ilisomeka bango lililobebawa na Njeri, ambaye alikuwa amevaa sare za shule

Kulingana na Omanga ni jambo la kusitikisha sana, na kusema kwamba atajitolea kumlipia mwanafunzi huyo ada ya shule.

"Haya yanavunja moyo! Kama mama imenivunja. Nimebaki nashangaa ni mazungumzo tu wakati tu Wizara ya Elimu inasema hakuna mwanafunzi anayepaswa kufukuzwa kwa sababu ya ada ya shule? Usawa wa ada ya 29,177 unaweza kupangwa kwa urahisi na NGAAF, CDF au hata bursary ya Kaunti.

Natafuta huyu msichana tafadhali nitumieni namba ya simu ya wazazi wake ama mmelete ofisini mwangu KICC,NINAENDA KULIPA ADA ZAKE ZA SHULE, NUNUA VIATU NA UPE MSAADA KWA UJUMLA," Aliandika Millicent.