Nilinyang'anywa mpenzi wangu na askari wa KDF-Mtumba man afichua haya

Muhtasari
  • Sande Mayua almaarufu Mtumba man amesimulia jinsi alikaribia kujiua baada ya kutupwa na mpenzi wake wa kwanza
  • Amekuwa akivuma baada ya video fupi za yeye akiuza nguo za mitumba kuenea
Mutuba man
Image: Hisani

Sande Mayua almaarufu Mtumba man amesimulia jinsi alikaribia kujiua baada ya kutupwa na mpenzi wake wa kwanza.

Amekuwa akivuma baada ya video fupi za yeye akiuza nguo za mitumba kuenea.

Yaliyokuwa na maana zaidi ni yeye akisema 'Ngara mpaka useme umepata mubaba.' na 'Nunua ya kukata msamaha.' 'nunua ya kuenda kumuona pasta.

Akiwa kwenye mahojiano, lisema kwama mpenzi wake alimuacha siku ya wapendanao mwaka wa 2013.

"Nilinyang'anywa mpenzi na askari wa KDF, tulikuwa pamoja kuanzia mwaka wa 2012, lakini mambo yalibadilika mwaka wa 2013

Ilikuwa siku ya wapendanao ambapo nilimnunulia maua ya 150, kumbe alikuwa ameenda kutembezwa na askari

Nililia wakati huo karibu nijiue, hapo ndipo nilifahamu mapenzi yanaua na ni ya kweli, nilifungiwa nyumba ya 1800 lakini nikarudi kijijini

NIlianza kuuza mitumba mwaka wa 2015, nimepitia mateso nilipokea simu kutoa kwa rafiki yangu akaniambia kwamba na vuma sana kwani nimepakiwa na vera sidika

Tulianza kuongea naye kwenye DM, Video ya kwanza nilichukuliwa na mwanamke rafiki yangu aliniambia kwamba anataka kuchua picha kumbe alicukua video," Alizungumza Mauya.

Pia alisema kwamba watu wengi wamekuwa wakimkejeli, kwa kuvalia mavazi ya wanawake.

"NImepokea kejeli nyingi kutoka kwa watu kwa sababu ya kuvalia nguo za wanawake, na hata wengi kusema kwamba mimi ni shoga, ukweli ni kuwa mmi sio shoga ni kazi tu nafanya, na napenda kazi yangu."

#PresenterAli #MayaudreamChaser