- Kuna baadhi ya changamoto ambazo watu wengi hupitia na kukata tamaa huku wengi wakiamua kutoa muamini Mungu
- Nikiwa katika ziara yangu nilikutana na kipusa ambaye alinisimulia masaibu ambayo alipitia kwenye maisha yake ya mapenzi
Kuna baadhi ya changamoto ambazo watu wengi hupitia na kukata tamaa huku wengi wakiamua kutoa muamini Mungu.
Sio mmoja au wawili bali asilimia kubwa ya watu wamekuwa wakikiri kwamba waliacha kumuamini Mungu kwa jambo moja au lingine.
Nikiwa katika ziara yangu nilikutana na kipusa ambaye alinisimulia masaibu ambayo alipitia kwenye maisha yake ya mapenzi.
KUlingana na kipusa huyo mpenzi wake alimuacha kwa mara ya kwanza, lakini akamrudia punde tu alipomuamini Mungu.
Huu hapa usimulizi wake;
"Katika maisha ya kupenda sijakuwa na bahati, kwani moyo wangu umejawa na uchungu mwingi, nilikuwa na huyu mwanamume ambaye tulikuwa tunapendana sana
Tulichumbiana kwa miaka miwili, mapema mwaka huu aliniambia kwamba tunapaswa kuachana kwani mimi sio ubavu wake, sikupinga lolote tuliachana kwa roho moja
Nilimuomba Mungu anifungulie nja na aweze kumrudisha mpenzi wangu kwani sikuwa tayari kumpenda mwanamume mwingine, ndio Mungu alijibu maombi yangu na imani yangu iliongezeka kwake
Miezi chache iliyopita aliniacha na kumwendea mwanamke mwingine, na hamna makosa mabayo nilitenda wala kumfanyia chochote
Kuanzia wakati ainiacha nilipoteza imani yangu kwa Mungu kwani sina furaha kamwe."
Je ni ushauri upi unapaswa kumpa mwanamke huyu, je azidi kumsubiria mpenzi wake au aendelee na maisha yake na kumrudia Mungu?