'Baby daddy wa kipekee katika maisha yangu,'Akothee kwa baby daddy anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari
  • Soma ujumbe wake Akothee kwa baby daddy anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Msanii Akothee ni miongoni mwa wanawake ambao wanawatambua baby daddy wao, na kuwapa heshima ambayo inayostahili.

Huku baby daddy wake akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alikumbuka maneno ambayo alimwambia baada ya kupatana naye.

Kulingana na Akothee baba wa watoto wake alimwambia kwamba atamlinda kama malkia, maneno ambayo alikiri hatawahi sahau maishani mwake.

"Kutoka siku uliyotuma macho yako kwangu! Wewe umeniambia jambo moja πŸ’‹ πŸ‘‰nitakufanya uwe malkia kwamba unapaswa kuwa, nitakuwa hapa kwa ajili yako mpaka kifo kitutenganishe)

Siwezi kusahau maneno yako wakati tulipoachana Maneno yako πŸ‘‰ (huna haja ya kuishi na watu unaowapenda, na haimaanishi wewe umeacha kuwapenda 😭😭😭😭, mimi daima nitakupenda Esta Mapenzi Yangu) naweza bado kujisikia joto lako, huduma na upendo.

Jaduonng πŸ™πŸ» Ninaweza kukimbia duniani kote bila kujali nikijua vizuri utanishika mkono, na kuwasaidia watoto wetu," Aliandika Akothee.

Aliendelea kumsifu na kusema kama unyenyekevu ungekuwa mtu angekuwa yeye, na kuongeza kwamba ni yeye baby daddy wa kipekee katika maisha yake.

" Unapofikisha 73 Papa Oyoo  Mungu akubariki mfalme. Ikiwa unyenyekevu ulikuwa mtu (hiyo ndiyo jaduonng yangu.)

Furaha ya kuzaliwa OSIEPNA. Baby daddy wa kipekee katika maisha yangu, ambaye hufanya co_oparenting kuwa rahisi. Anapigana kwa ajili yangu hata na baby daddy wengine kwake watoto wangu ni watoto wetu πŸ™πŸ»πŸ™πŸ»."