Chagua kiongozi wa kweli sio wanabiashara-Otile Brown awashauri wakenya

Muhtasari
  • Otile Brown awashauri wakenya kuwachagua viongozi wa kweli

Huku wakenya wakijitayarisha kuingia katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022, msanii Otile Brown kupitia kwenye ukurasa wake amewashauri wakenya kuchagua kiongozi wa kweli.

"Wakati mwengine sisi wa Africa ndio chanzo cha matatizo yetu...we've suffered for looong because of our own selfish decisions," UJumbe wake ulisoma.

Tumwaona baadhi ya vigogo humu nchini wakipigana kwa vita vya maneno mitandaoni na hadharani kwa jambo moja au lingine.

Otile aliwashauri wakenya endapo mtu anachukua hongo hilo ni kutesa rafiki yake na mtoto wake.

Kwa muda mrefu kenya imekumbwa na ufisadi, na siasa za kabila jambo ambalo Otile amewashauri wakenya kuachana nayo.

"Kuchagua viongozi kisa ufanatic, mtu wetu na kuhongwa ni ushamba,Kenya tunaweza ishi kama ulaya na sote tunajua hilo, uwezekano upo...weka hisia zako, mapenzi ya jamii yako na kiburi kando natufanye waamuzi wa akili

Mabadiliko yanaanzia kwako wewe mpiga kura...Chagua kiongozi wa kweli na sio wanabiashara."

Usemi wake unajiri siku moja baada ya mfanyibiashara Wanjigi ushambuliwa siku ya Ijumaa.

Msanii huyo aliendelea na ujumbe wake na kusema kuwa;

"Nina imani wengine tumejanjaruka , tumekomaa , tumejifunza , tumekua ila wakati mwengine na waangalia vijana wenzangu wanayofikiria na wanavyoendeshwa na vitu visivyokua na msingi kisha nasikitika... It’s like we don’t want what’s good for us ..

Life is about choices… Hayo matitzo huenda unapitia sahii pengine hayangekuepo tusingeendeshwa na tamaa , ubinfsi , ukabila na ujamaa ❤️🇰🇪," Otile Aliandika.