'Mwanamke sio mbuzi eti apende majani,'Ushauri wake Nyota Ndogo kwa Wanaume

Muhtasari
  • Nyota Ndogo aibua hisia mseto baada ya kusema hakuna mwanamke hapendi pesa
Nyota Ndogo
Nyota Ndogo
Image: Instagram

Mwanamuziki Mwanaisha Abdalla maarufu Nyota Ndogo kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook, amewakomesha wanaume wote ambao wamekuwa wakiwaacha wapenzi wao kwa madai kwamba wanapenda pesa.

Kulingana na mwanamuziki huyo hamna mwanamke ambaye hapendi pesa, na hakuna mahali unaweza mpata mwanamke hapendi pesa.

Pia aliedelea na ujumbe ake na kusema kwamba wanawake sio mbuzi wanategema majani kula.

"BRO. usimuache mwanamke wako kwasababu anapenda pesa. wote wako hivyo hivyo. Mwanamke sio mbuzi eti apende majani," Aliandika Nyota.

Ni ujumbe ambao uliibua hisia mseto kwenye mitandao, na hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;

Idias Koll: yNa wewe usimuache boy wako ju anapenda mademu...yeye sio gay apende wanaume wenzake

ROSY mamake waitherero:  · NYOTA NDOGO Kuna siku fafa waitherero aliniambia eti napenda pesa kumliko nikamwambia ajiangalie vizuri aone vile anakaa Kama nugu Kama sio pesa Kama ningekuwa na yeye🙆🙆Kama njeri Kia mbaa,mukami Kia ndore na kile kimama Kinono Kia karumaindo flats wangekuwa vifaranga wake wa kando Alaaah🤷🤷 pesa ni sabuni ya roho❣️

Kennedy Opio: Kupenda pesa sivibaya, lakini wanawake wasikuhizi wanapenda pesa sana mpaka wanasahau wakokwa ndoa

Sajopesh Okwaro: Haha Ivo ndo munafanya mabwana za watu WANAKUFA maskini,,,,,,,mbona musieke akili pamoja mujenge boma

Binrajab Athman: Mwapenda pesa na ajabu hamupati utajiri zaidi ya kupata mimba kama panya

Dauglas Mogoi: Before upende yangu wewe hupata ngapi at the end of the day or a month,,,, because what I can do you can do better.... I can't be a bank account for an idler...