Mungu ameyafuta machozi yenu,'Mchekeshaji DR Ofweneke awapongeza Mulamwah na mkewe

Muhtasari
  • Mchekeshaji DR Ofweneke awapongeza Mulamwah na mkewe
  • Wawili hao walitangaza kuzaliwa kwa binti yao ambaye wamempatia jina Keilah Oyando kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii
Image: INSTAGRAM// MULAMWAH

Mchekeshaji David Oyando almaarufu kama Mulamwah na mpenzi wake Caroline Muthoni wamekaribisha mtoto wao wa kwanza duniani.

Wawili hao walitangaza kuzaliwa kwa binti yao ambaye wamempatia jina Keilah Oyando kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.

"Na ni msichana. Muujiza umewasili.. maneno hayaweza kueleza ninavyohisi, ni kitu cha maana zaidi kuwahi fanyika maishani mwangu. Karibu kipenzi @keilah_oyando" Mulamwah aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Msanii huyo ambaye pia ni muuguzi alichukua  nafasi ile kumshukuru mpenzi wake na kumbubujikia sifa kufuatia hatua hiyo.

"Asante mpenzi @carrol_sonie kwa zawadi nzuri. Wewe ni mwanamke jasiri kuweza kufanya haya licha ya yale yote tumepitia. Asante sana kwa waliotutakia mema na kutuombea. Asanteni sana" Mulamwah alisema.

Baadhi ya wanamitandao waiwapongeza wapenzi hao, huku mchekeshaji DR Ofweneke akiwapongeza na kuwaambia kwamba Mungu ameyapanguza machozi yao.

Mulamwaha na mpenzi wake walimpoteza kifungua mimba wao mwaka jana, huku wakiwa kwenye mahojiano na Radiojambo, Sonie alisema hajawahi fahamu nini haswa kulimtendekea mwanawe.

"🦅🦅🦅the eagle🦅🦅🦅 :: @Mulamwah & @carrol_sonie Mungu kwa hakika ameyafuta machozi yenu,mnaposherehekea  kuwasili kwa kifungu chenu cha baraka, Mungu awape hekima ya asili na nguvu & neema ya kutoa !! :: Hongera!" Aliandika Ofweneke.