'Ninajivunia,'Guardian Angel afichua aliyoyapitia baada ya kutangaza uhusiano wake na mpenziwe

Muhtasari
  • Guardian Angel afichua aliyoyapitia baada ya kutangaza uhusiano wake na mpenziwe

Msanii wa nyimbo za injili Guardian Angel, alivuma mwaka jana baada ya kutangaza uhusiano wa kimapenzi a Esther Musila.

Kilichowachangia wanamitandao kukejeli uhusiano wake, ni kwa ajili yatofauti iliyoko kwenye umri wao.

Lakini hawakukosea waliposema 'Age is just but  a number'.

Kuna baadhi yao ambao waliwapongeza, lakini wanamitandao hawawezi kosa jambo la kukejeli.

Guardian na Esther walifichua kwamba walipatana kwenye sherehe moja ambapo walitambulishwa na mmoja wa marafiki zao.

Wawili hao wamekuwa mitandaoni, wakiwapa wanamitandao mfano mwema jinsi ya kuishi kama wapenzi na wanandoa.

Leo (Jumatatu) msanii huyo ameamua kujisifu kwa kuwa na moyo wenye ujasiri, na kutosikiza kejeli za wanamitandao.

Kulingana na Angel kama angesikiza kejeli kelele za watu angepoteza zawadi ya kipekee.

"Kama ningesikiza kelele zao ningepoteza zawadi maalum,ninajivunia," Aliandika Guardian.

Kwa kweli wawili hao hawajakuwa wakisumbuliwa na kejeli za wanamitandao, kwani mapenzi yao yamekuwa yakinoga kila kuchao.

Baada ya ujumbe wake Guardian Angel, mkewe alimjibu na kumwabia kuwa;

"Awww G yangu, usiwe na hisia mbaya kwa kufanya uamuzi kuhusu maisha yako mwenyewe ambayo huwapa watu wengine

Wewe sio wajibu wa furaha yao. Unawajibika kwa furaha yako mwenyewe. Mtu yeyote ambaye anataka wewe kuishi katika taabu kwa furaha yao haipaswi kuwa katika maisha yako kuanza. Ninajivunia ❤️,"Alijibu Esther.