'Baada ya kipindi nilikuwa nalia,'Nana Owiti afunguka kuhusu ugonjwa wa mumewe King Kaka

Muhtasari
  • Baada ya rappa King Kaka kufahamisha mashabiki wake kwamba alikuwa mgonjwa kwa miezi 3 wanamitandao,mashabiki na marafiki walimtakia afueni ya haraka
  • Nana Owiti afunguka kuhusu ugonjwa wa mumewe King Kaka
90226946_2651278888481699_8770703791842362787_n (1)
Nana Owiti 90226946_2651278888481699_8770703791842362787_n (1)
Image: Instagram

Baada ya rappa King Kaka kufahamisha mashabiki wake kwamba alikuwa mgonjwa kwa miezi 3 wanamitandao,mashabiki na marafiki walimtakia afueni ya haraka.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram siku ya Jumatatu, alimshukuru mkewe mtangazaji Nana Owiti kwa kusimama naye wakati huo mgumu.

Huku Nana akijibu ujumbe wa mumewe, ameweka wazi kwamba baada ya kumaliza kipindi, alikuwa anaenda kwenye chumba cha mapodozi na kuanza kulia, kwa ajili ya mumewe.

Pia alisema kwamba halikuwa jambo rahisi kwani alikuwa anaficha uchungu, na kuvunjika moyo wakati mwingi, ili kumtia mumewe nguvu na kumpa matumaini.

"Mara tu nilipomaliza kipindi nilikuwa naenda katika humba cha mapodozi nilisuburi kila mtu aondoke ili niweze kulia @fredmuitiriri alinipatia usiku mmoja ..

kwa wote, nilipaswa kuwa na nguvu kwa ajili yenu hata ingawa hiyo inamaanisha 'kuifanya' sana Sikuweza kukuonyesha kukata tamaa. Nilikuwa nakupa tumaini. Ninakupenda milele! ❤️❤️❤️," Nana alijibu.

 

Kulingana na King Kaka mkewe alionyesha kuwa mwanamke, na rafiki ni nini, wakati wa kipindi hicho alichokuwa mgonjwa.

"Napenda kuhesabu baraka zangu. Miezi 3 iliyopita hakuwa na kitu cha muda mfupi lakini cha kutisha, mwanamke huyu hapa @nanowiti ameonyesha na kuthibitishwa nini mke na rafiki bora ni.

Kutoka Kulala Kwakiti cha Hospitali karibu na kitanda changu basi wewe kuamka oga katika hospitali hiyo, kwenda na kutabsamu kwa runina  kama kila kitu ni sawa kupigana na wauguzi kwa nini wao wanfanya kazi polepole (asante kwa wauguzi ambao walinitunza, ni vile Nana alikuwa anataka nipone haraka) Kuomba na kunitia moyo ni kule