Mume wangu aliniacha baada yangu kuwa kiwete-Mwanamke asimulia

Muhtasari
  • Nikiwa kwenye ziara yangu, nilipatana na mwanamke mmoja ambaye alinisimulia hadithi yake na sababu kuu ya kauchana na mumewe
  • Kulingana naye walifunga ndoa na mumewe, katika harusi ya kipekee na kubarikiwa na watoto wawili
sad woman
sad woman

Kuna baadhi ya watu ambao walizaliwa na kukua wakiwa sawa, lakini jambo moja au lingine mbaya likawatendekea na kubadili maisha yao.

Nikiwa kwenye ziara yangu, nilipatana na mwanamke mmoja ambaye alinisimulia hadithi yake na sababu kuu ya kauchana na mumewe.

Kulingana naye walifunga ndoa na mumewe, katika harusi ya kipekee na kubarikiwa na watoto wawili.

Lakini alifanya nini ili awachane na mumewe, na sababu yake ya kuwa kiwete ni ipi? licha yake kuzaliwa akiwa vyema.

Huu hapa usimulizi wake;

"Unapo niona hivi nilizaliwa nikitembea yema,sikuzaliwa nikikalia kiti hiki cha kiwete, nilikuwa na mume ambaye alikuwa ananipenda sana

Tulikuwa kwa ndoa kwa mia 5, tulikuwa tumebarikiwa na watoto wawili. sababu yangu kuu ya kuwa kiwete, ilipata ajali kitinda mimba wangu akiwa na miezi 6

Nilitibiwa lakini baada ya mwaka mmoja mume wangu aliniacha na kuniachia watoto wawili, si kuwa na uwezo wowote, lakini dada yangu alinisaidia na ni yeye amekuwa akinisaidia 

Mika 4 imepita baada ya kuniacha na sijui anaendelwa vipi, na wala hajawahi tujulia hali jinsi tunavyoendelea, na anafahamu vyema nina watoto wake

Yaani wanaume wengine ni kama waliumbwa na shetani na wala sio Mungu ambaye anatuwezesha,furaha yangu ni kuwaona watoto wangu wakiendelea vyema na wakiwa na afya," Alieleza Mwanamke huyo.