'Niombeeni,'Weezdom awaambia mashabiki,huku akisema yuko hospitalini

Muhtasari
  • Msanii Weezdom na aliyekuwa meneja wa msanii Bahati kupitia kwenye ukurasa wa instagrama amewafahamisha mashabiki wake kuwa ni mgonjwa

Msanii Weezdom na aliyekuwa meneja wa msanii Bahati kupitia kwenye ukurasa wa instagrama amewafahamisha mashabiki wake kuwa ni mgonjwa.

Weezdom amekuwa akitoka kibao kimoja baada ya kngine huku baadhi ya vibao vyake vikipendwa sana na mashabiki.

KUpitia kwenye ujumbe wake alioandika mitandaoni hakufichua anaugua nini,bali alisema amekuwa na maumivu usiku kucha.

Aliwaambia mashabiki wake wamueke kwa maombi yao ili aweze kupona.

"Nimekuwa na maumivu jana si kulala hadi kukakucha, nashukuru Mungu kwa sasa niko hospitalini natibiwa, maisha ni ya muimu sana, niombeeni," Aliandika Weezdom.