Bilionea Grand P avunja kiuno chake akijiburudisha na mpenzi wake mwanasoshalaiti Eudoxie Yao

Muhtasari

•Kulingana na ripoti mbalimbali,  Grand P anahudumiwa katika hospitali ya Metro nchini Guinea baada ya kulalamikia maumivu kwenye kiuno chake siku chache tu baada yake kuonekana akijiburudisha na mpenzi wake mwenye maumbile makubwa kweli.

Image: HISANI

Mwanamuziki mashuhuri kutoka Guinea Moussa Sandiana Kaba almaarufu kama Grand P anaripotiwa kulazwa hospitalini baada ya kuugua kwenye kiuno chake alipokuwa anajiburudisha na mpenzi wake mwanasoshalaiti Eudoxie Yao.

Ripoti mbalimbali zinasema kwamba Grand P anahudumiwa katika hospitali ya Metro nchini Guinea baada ya kulalamikia maumivu kwenye kiuno chake siku chache tu baada yake kuonekana akijiburudisha na mpenzi wake mwenye maumbile makubwa kweli.

Wiki chache zilizopita video na picha zilizoonyesha mwanasoshalaiti Yao akiwa amemkalia Grand P zilienezwa sana mitandaoni.

Kwenye video ambayo Grand P alipakia katika ukurasa wake wa Instagram, wapenzi hao wawili walionekana wakishiriki densi huku Yao akiwa amemkalia mbwenyenye huyo.

Inadaiwa kuwa kipindi hicho cha burudani ndicho kilisababisha maumivu makali kwenye kiuno cha msanii huyo mwenye maumbile ya kipekee hadi akapatwa na matatizo ya kusimama imara.