Kwa nini Harmonize amelazimika kufuta ziara yake ya Canada na Uswidi

Muhtasari
  • Kwa nini Harmonize amelazimika kufuta ziara yake ya Canada na Uswidi
Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Msanii Harmonize amelazimika kufuta na kuahirisha ziara yake ya muziki katika nchi ya Canada na Uswidi.

 Konde boy alikuwa amepangwa kuwatumbuiza mashabiki wake  huko Canada mnamo Oktoba 30 na nchini Sweden mnamo Novemba 6, lakini ziara yake imeahirishwa.

"Watu wa Damu yangu  huko Canada & Sweden 🇨🇦 & 🇸🇪naomba msamaha kwa maana sitaweza kufanya ziara yangu kama ilivyo kwenye tarehe ya kalenda aua ratiba yetu 😢 kutokana na vikwazo vya covid-19kwa hivyo nitawaarifu  mashabiki wangu wote waaminifu ASAP kwenye tarehe mpya ya ziara kwa mtu yeyote ambaye ana tiketi niamini nitakuwa huko Mungu akipenda

Angalia na mvulana wangu @ dj.storm6 Hebu tuende 🚶 Las Vegas 24/9 / New York 1/10 / La 9/10 / Boise Idaho 15/10 Minissota 22/10 na zaidi .... !!!!! " Alisema Harmonize.

Hata hivyo, licha ya kufuta ziara hiyo , Meneja wa Harmonize aliwahakikishia mashabiki wao hukouswidi na Canada kuweka tiketi zao kwani watatangaza tarehe mpya hivi karibuni.