Wacha kuharibu wakati wako na watu hawakujali-Boniface Mwangi

Muhtasari
  • Kwa hakika hatuwezi chagua watu ambao tutapatana na wao katika maisha yetu, lakini tuna jukumu kubwa la kuchagua watu ambao watahusika maishani mwetu
Boniface Mwangi
Image: Hisani

Kwa hakika hatuwezi chagua watu ambao tutapatana na wao katika maisha yetu, lakini tuna jukumu kubwa la kuchagua watu ambao watahusika maishani mwetu.

Jambo kubwa ambalo watu wengi wamesalia kwenye uhusiano duni au ndoa zenye vurugu ni uchaguzi mbaya wa marafiki na wenzi wetu.

Kuna baadhi ya watu na hata jamaa zetu ambao wamekuwa wakijali sana na maisha ya jamaa na marafiki zao, lakini wakitarajia hayo kutoka kwa marafiki hao inakuwa kinaya.

Mwanaharakati  Boniface Mwangi, baada ya kuchukua mapumziko kutoka kwa siasa, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amekuwa akiwapa mashabiki wake ushauri.

Kulinagana na ushauri wa awali wa Boniface amewashauri mashabiki wake wawache kuharibu maisha yao na watu ambao hawawajali.

"Wacha kuharibu wakati wako na maisha yako na watu ambao hawakujali," Alisema Boniface.

Je umewahi japata katika hali kama hii unajali kuhusu watu wengine, lakini unapowahitaji tena hautawapata na wala hawakujali?

Boniface Mwangi
Image: Hisani