"Hata hawezi kula kama siko naye mezani" Vera Sidika asifia mapenzi makubwa anayoonyeshwa na mumewe Brown Mauzo

Muhtasari

•Mwanasoshalaiti huyo mzaliwa wa Mombasa ameendelea kumbubujikia mumewe sifa tele siku moja baada ya nyingine na kuwaacha wasio na wachumba wakimeza mate tu.

•Vera amesema kuwa baada ya kuhangaishwa na mapenzi kwa miaka mingi hatimaye amebahatika kupata kipenzi cha maisha yake.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Kama kuna jambo bora zaidi kuwahi fanyikia mwanasoshalaiti mashuhuri Vera Sidika ni hatua ya kufunga ndoa na mpenzi wake  Brown Mauzo kama inavyoashiriwa na matendo yake mitandaoni.

Mwanasoshalaiti huyo mzaliwa wa Mombasa ameendelea kumbubujikia mumewe sifa tele siku moja baada ya nyingine na kuwaacha wasio na wachumba wakimeza mate tu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vera amesema kwamba Mauzo ni kila kitu alichoomba Mungu na kudai kwamba angependa kujenga familia naye.

Vera amesema kuwa baada ya kuhangaishwa na mapenzi kwa miaka mingi hatimaye amebahatika kupata kipenzi cha maisha yake.

"Nyote ambao mmenifuata kwa miaka mnajua nimekuwa na wakati mgumu kwenye mahusiano. Woi. Lakini Mungu ni nani?? Kwa kweli kila mtu amehifadhiwa mtu wake. Napenda mwisho mwema" Vera alisema.

Vera amezungumzia mapenzi makubwa ambayo mumewe anamtunza nayo na kudai kwamba hata hawezi kakubali kula kama hawako pamoja.

"Bae ni mtu wa kushangaza sana. Hata hawezi kula chakula kama hatuko na yeye mezani. Hata kama sijiskii kula, lazima nikuwepo. Nikae tu nimtazame. Mimi ndiye hamu yake ya kula. Jamaa anaweza kunitoa kitandani na kunipeleka katika chumba cha maakuli muradi tu akule" Vera amesema.

Amewashauri wale ambao wamekuwa wakihangaika kwa sababu ya mapenzi wasikate tamaa  kwani mwishowe watabahatika kama yeye.