Najutia kuavya mimba mara 6,nilikuwa nataka kujifurahisha maishani-Mwanamke akiri

Muhtasari
  • Akina babu zetu walisema kwamba mtoto ni baraka kutoka kwa Mungu lakini kuna wanawake wale ambao hawafahamu wala kutambua msemo huo
  • Kama tunavyojua kuavya mimba ni makosa na wala sio halali, na kulingana na amri za biblia utakuwa muuaji
black-woman-crying-
black-woman-crying-

Akina babu zetu walisema kwamba mtoto ni baraka kutoka kwa Mungu lakini kuna wanawake wale ambao hawafahamu wala kutambua msemo huo.

Kama tunavyojua kuavya mimba ni makosa na wala sio halali, na kulingana na amri za biblia utakuwa muuaji.

Hata hivyo baadhi ya wanawake wamekuwa wakiavya mimba kila kuchao, kwani hawayuko tayari kupata majukumu.

Nikiwa kwenye zizra zangu, mwanamke mmoja alinisimulia jinsi awali ameavya mimba 6, na hata kuolewa na wanaume 7.

Anachojutia maishani mwake ni kuavya mimba, kwani ni jambo ambalolimemletea shida katika maisha yake ya ndoa.

"Mimi, nimeolewa mara 7, pia niliavua mimba mara 6, pia nilifungwa jela kwa wiki mbili baada ya kupatikana na mume wa mtu

Najutia kuavya mimba kwani nimekuwa kwa ndoa yangu sasa kwa miaka 2 na nusu na sijapata mtoto, wazazi wa mume wangu au wakwe wangu wamekuwa wakilalamika kwani sijawaletea wajukuu

Pia najutia mambo mabaya yote ambayo nimekuwa nikitenda awali, naomba tu Mungu angenipa mtoto mmoja nishukuru, nilifanya hayo yote kwa maana sikuwa tayari kwa majukumu, na nilikuwa nataka kujifurahisha maishani," Alieleza Jennifer.

KIla jambo lina majuto yake na matokeo yake.