Nimemfunga mpenzi wangu na dawa ya mganga-Mwanamume akiri

Muhtasari
  • Wakati huu mambo yameenda kinyume na matamshi ya wengi, kwani wanaume wengi wamekiri kuenda kwa waganga ili waweze kupendwa na wanawake wao
  • Je siku na karne hii ya sasa kuna mapenzi ya kweli, kama ya enzi za akina babu zetu?

Wengi husema na kudai kwamba asilimia kubwa ya wanawake ndio huenda kwa mganga kwa ajili ya mapenzi.

Wakati huu mambo yameenda kinyume na matamshi ya wengi, kwani wanaume wengi wamekiri kuenda kwa waganga ili waweze kupendwa na wanawake wao.

Je siku na karne hii ya sasa kuna mapenzi ya kweli, kama ya enzi za akina babu zetu?

Katika sekta ya mapenzi, mjadala umeibuka kila kuchao kila jinsia ikilaumu jinsia ile nyingine.

Kuna wale wanasema kwamba wanawake wanapenda pesa na wala hawaonyeshi mapenzi ya kweli, huku wanawake wakisema kwamba wanaume wanawapenda wanawake wengi yaani wanapenda mipango ya kando.

Mwanamume mmoja aliwaacha wengi midomo wazi baada ya kusimulia jinsi amemfunga mpenzi wake.

"Nilienda kwa mganga ili mpenzi wangu asiniache, aliniambia nimpelekee chupi yake, nilimpeleka na nikapewa dawa ya kumfunga ili anipende

Kuna wakati aliniuliza ni nini nilimfanya nimpende, na mwambia ni mapenzi ya kweli," Alieleza Jamaa huyo.

Je umefanya ujinga upi kwa ajili ya mapenzi?