"Nimeingia Nairobi jana na nikaibiwa kweli" Mwanamuziki Nyota Ndogo asimulia jinsi alivyotapeliwa

Muhtasari

•Mzaliwa huyo wa Pwani amesema kwamba alivutiwa sana na bidhaa ambazo aliona  zikiuzwa mitandaoni na bila kusita akatumia 'muuzaji' yule ujumbe akitaka kujua zaidi kuzihusu ili azinunue.

•'Muuzaji' yule alimhakikishia Nyota kwamba angeweza kupokea bidhaa alizonunua kabla ya saa moja usiku kutimia lakini do! baada ya masaa ambayo walikubaliana kupita alipigwa na butwa kugundua kuwa alichokuwa amesubiri ni kupata na uyakinifu kwamba alikuwa kachezwa tu.

Image: INSTAGRAM// NYOTA NDOGO

Mwanamuziki mashuhuri Nyota ndogo amesimulia alivyopoteza pesa zake kwa mlaghai aliyejifanya muuzaji viatu mitandaoni siku ya Jumanne.

Kupitia mtandao wake wa Instagram, Nyota Ndogo amesema kwamba anajilaumu mwenyewe kwa kutokuwa makini alipokuwa anatapeliwa bila kugundua.

Mzaliwa huyo wa Pwani amesema kwamba alivutiwa sana na bidhaa ambazo aliona  zikiuzwa mitandaoni na bila kusita akatumia 'muuzaji' yule ujumbe akitaka kujua zaidi kuzihusu ili azinunue.

"Jana wololoyayeeee nimeoshwa mimi. Nimeona vitu vizuri kwa ukurasa hapa Instagram akaja WhatsApp nikamtumia vitu nataka kwa upumbavu wangu mwenyewe akaniambia nitume pesa kwa namba nyingine akasema itakuja jina Faith na kweli nikatuma shilingi elfu sita" Nyota Ndogo alisimulia.

'Muuzaji' yule alimhakikishia Nyota kwamba angeweza kupokea bidhaa alizonunua kabla ya saa moja usiku kutimia lakini do! baada ya masaa ambayo walikubaliana kupita alipigwa na butwa kugundua kuwa alichokuwa amesubiri ni kupata na uyakinifu kwamba alikuwa kachezwa tu.

"Alisema kwamba vitu zitakuja saa moja usiku maana nilikuwa natoka saa mbili. Nyota mimi nilikula block Insta, kula block WhatsApp. Huyu Faith kwanza ananikatia simu" Nyota alisimulia,

Mwanamuziki huyo amesema kwamba anaumwa sana na pesa alizopoteza kwani alikuwa amezifanyia kazi kwa bidii.

Amewatahadharisha wanamitandao wengine wasije wakaanguka kwenye mtego ule ule uliomnasa akajipata akienda hasara.

Nyota amesema kwamba amekuwa akiagiza bidhaa zake mitandaoni na kamwe hajawahi kutapeliwa tena ila jana haikuwa siku yake ya bahati.