'...Tabu unazopitia leo kuna siku zitaisha,'Diamond awashauri mashabiki wake

Muhtasari
  • Staa wa bongo Diamond Platnumz ni miongoni mwa wasanii ambao wamefanikiwa maishani Afrika mashariki
Diamond

Staa wa bongo Diamond Platnumz ni miongoni mwa wasanii ambao wamefanikiwa maishani Afrika mashariki.

Diamond amekuwa kwenye tasnia ya muziki kwa zaidi ya miaka 10, huku licha ya changamoto anazopitia akijitahidi na kutoa kibao kimoja baada ya kingine.

Vibao vyake vimekuwa vikipokea zaidi ya watazamaji milioni moja kwenye youtube.

Pia ni msanii ambeye amekuza vipaji vya wasanii wenzake, na kufanya collabo na wasanii tofauti sio Afrika pekee bali wasanii wa nchi tofauti ulimwenguni.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instaram staa huyo amepakia video ya kibao cha 'Kamwambue' ambacho alifanya kabla ya kuwa maarufu sana na kuwashauri mashabiki wake wasikate tamaa.

Kulinga na Diamond taabu ambazo mtu anapitia leo kuna siku zitaisha, licha ya yote wanaaswa kutia bidii katika kazi zao na kuwa na heshima.

"Kila Unapojihisi kukata tamaa play hii nyimbo, ikukumbushe kuwa tabu unazopitia leo kuna siku zitaisha.. Sali sana, Ongeza bidii na Ubunifu kwenye ulifanyalo, Muheshim kila mtu na Mwenyez Mungu atakufungulia 🙏🏼," Diamond aliandika.

Msanii huyo amekuwa akitegemea usanii wake, sio kama baadhi ya wasanii ambao wanategemea biashara na usanii wao kwa wakati mmoja.

Kwa hivyo tunaweza usema kwamba licha ya yote ametia bidii, na amekuwa mfano mwema kwa vijana wa kisasi cha sasa.