Hizi hapa sababu kuu kwa nini wakenya wanapenda ndoa za 'come we stay'

Muhtasari
  • Hizi hapa sababu kuu kwa nini wakenya wanapenda ndoa za 'come we stay'

Iichukie au iipende,ndoa za 'come we stay' iko hapa kukaa. Mpangilio huu usio rasmi wa wanandoa wanaokaa bila malipo ya mahari, wakishirikiana na rundo la suti zinazoliwa na nondo zilizopigwa na hali ya hewa, ni maarufu zaidi.

Asilimia kubwa ya wanandoa nchini walianza ndoa kama 'come we stay'.

Nikiwa kwenye ziara yangu, nilipatana na wanaume ambao walikuwa wanajadiliana kwa nini wakenya wengi au asilimia kubwa ya wanandoa wanapenda ndoa za 'Come we stay'.

Asilimia kubwa walikuwa wanalalamika kuhusu kulipa mahari, huku wengi wakisema kwamba walijipata tu wamenzisha ndoa na wapenzi wao.

Lakini hizi happa sababu kuu kwa nini wakenya wanapenda ndoa za 'come we stay'

1.Mahari ni ya gharama kubwa

Wanaume wa Kenya wanachukia harusi. 'come we stay' huwaokoa kiwewe cha kushughulika na mazungumzo mazito ya mahari na mipango ya harusi. Hakuna haja ya karamu na karamu za kula mbuzi ili kukusanya pesa kwa ajili ya harusi.

2.Dhobi 

Wakati mpenzi wako ameamua kuishi nawe na kuanzisha ndoa pamoja, ni wakati wa kumwambia 'mama fua' kwaheri kwani kazi yake itakuwa ikifanywa na mpenzi wako.

Kwa  hivyo hamna haja ya kuharibu pesa ya kulipa mama fua.

3.'Ball' bila stress

Kwa maana ameaamua kuisi nawe haya basi mwanamke wako ata hakikisha kwamba amepata ujauziro, na kisha hutakuwa na mawazo kwani anaishi nawe.

Hii ni tofauti na kile unampa mpenzi wako ujauzito bali anaishi na wazazi wake, kwa hivyo ina maana una maswali ya kujibu.

4.Lungula

Ni ndoa ipi ambayo ina dumu bila haki ya kitandani? hamna, kwa hivyo ukimuoa mpenzi wako utakuwa ukipata haki yako bila ya kutuma 'fare' wala kukaa sana bila kufanya tendo la ndoa.

Je ni sababu zingine zipi ambazo zinazoonyesha kwa nini wakenya wanapenda ndoa ya 'Come we stay'.