'Niliwaambia wavuke sakafu,'Eric Omondi awaambia Babu Owino na Jaguar kujiunga na Jimmy Wanjigi

Muhtasari
  • Baada ya mchekeshaji huyo kumpigia debe Jimmy amekuwa akipokea kejeli nyingi kutoka kwa mashabiki na wakenya kwa jumla
  • Huku akianzisha kampeni, Eric alisema ni wakati wa vijana kuongoza nchi na kuanza mwamko mpya

Licha ya Eric Omondi kuwa mchekeshaji maarufu nchini, amekuwa akimpigia mwanabiashara Jimmy Wanjigi debe.

Kauli kuu ya Eric Omondi ni 'Fagia wote'.

Baada ya mchekeshaji huyo kumpigia debe Jimmy amekuwa akipokea kejeli nyingi kutoka kwa mashabiki na wakenya kwa jumla.

Huku akianzisha kampeni, Eric alisema ni wakati wa vijana kuongoza nchi na kuanza mwamko mpya.

KUpitia kwenye ukurasa wake wa instaram,amepakia picha akiwa na mbunge wa Embakasi Babu Owino na mbunge wa Starehe Jaguar.

Katika ujumbe wake alidai kwamba aliwaambiwa wawili hao wajiunge na chama cha bosi wake Wanjigi kwa mwendo upole.

"Nimetembelewa hapa kwangu State House Karen na Waheshimiwa Vijana @he.babuowino and @jaguarkenya Nimewaambiwa wavuke sakafu Kwa mwendo wa Aste aste waje upande huu wa FAGIA WOTE!!!#FagiaWote," Aliandika Eric.

Je kwa maoni yako Eric alifanya vyema kujiunga na siasa au amepoteza mwelekeo wa kazi yake ya uchekeshaji?