Janet Otieno afichua sababu ya baba yake kukaa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti kwa miezi 2

Muhtasari
  • Janet Otieno afichua sababu ya baba yake kukaa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti kwa miezi 2
janet otieno
janet otieno

Ktika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye msanii wa nyimbo za injili Janet Otieno, ambaye alifichua sababu kuu ya baba yakae kukaa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti kwa muda wa miezi 2 bada ya kuaga dunia.

Janet amekuwa akitoa kibao kimoja baada ya kingine, huku akifichua kwamba amekuwa akitoa vibao vyake kulingana na matakwa ya mashabiki wake.

Mwezi wa JUni Janet alimpoteza baba yake, ambaye amesema kwamba walikuwa katika nadoa na mama yake kwa zaidi ya miaka20.

Mazishi yake yalikawia sana, huku msanii huyo akisema kwamba familia yake iliambukizwa na virusi vya corona.

"Baada ya baba yangu kuaga dunia, tulienda nyumbani mimi na ndugu zangu kuenda kupanga mazishi, baada ya kurudi nilianza kupata dalili za corona

Nilipoenda hospitali niliambiwa kwamba nina homa ya matumbo, siku kadhaa baadaye mue wangu aliana kuwa mgonjwa tulipoenda hospitalini tulipmwa maambukizi ya corona na tukapatikana na virusi hivyo

Familia yote kwa jumla tuliambukizana, na hiyo ndio sababu kuu baba yangu alikaa sana kwenye chumba cha kuhifadhi maiti, yaani mazishi yake yalichukua miezi 2 kwa sababu ata baada ya kupona hatukuwa na nguvu vile," Alieleza Janet.