Mchezaji filamu maarufu wa Nigeria Chiwetalu Agu akamatwa

Muhtasari

•Kulingana na taarifa kutoka makao makuu ya jeshi wamemkamata wakati walipokuwa wakifanya msako wa wafuasi wa genge linalounga mkono jamii ya wazawa ya Biafra wanaotaka kujitenga nchini humo (IPOB).

Image: OTHERS

Jeshi la Nigeria limethibitisha kumkamata mchezaji wa filamu wa N Nollywood Chiwetalu Agu.

Kulingana na taarifa kutoka makao makuu ya jeshi wamemkamata wakati walipokuwa wakifanya msako wa wafuasi wa genge linalounga mkono jamii ya wazawa ya Biafra wanaotaka kujitenga nchini humo (IPOB).

Taarifa hiyo imeeleza pia kwamba mchezji filamu huyo alichukuliwa alipokuwa amefaa nguo zinazotambulisha kikundi hicho kwa ajili ya kumuhoji na ingawa alionyesha pingamizi, jeshiu limefanya juhudi za kumuweka mahabusu , na linasema halikumyamyasa wala kumtesa.

Taarifa hikyo imeongeza kuwaingawa jeshi linatambua haki za raia wote za kutembea kwa uhuruna kujieleza kama haki yao ya kikatiba, halitakubali ukiukaji wa wa sheria wa mtu binafsi au kikundi kwa kuchochea umma kufanya ghasia au kuvunja sheria na utulivu.

Biafra ni nini?

Kikundi kinachotaka kujitenga kiitwacho Watu wa Asili wa Biafra kimekuwa kikipambana na vyombo vya usalama vya Nigeria. Kundi hilo linataka eneo fulani kusini-mashariki lenye watu kutoka kabila la Igbo, wajitenge na kuunda taifa lao huru la Biafra. Kundi hilo lilianzishwa mnamo mwaka 2014 na Nnamdi Kanu, ambaye alikamatwa na kukabiliwa na mashtaka ya ugaidi na uhaini.