'Asanteni kwa kusimama nasi,'Size 8 awashukuru wote waliosimama naye baada ya kumpoteza mwanawe

Muhtasari
  • Msanii wa nyimbo za injili Size 8 amewashukuru wote abao walisimama nap baada ya kumpoteza mtoto wake

Msanii wa nyimbo za injili Size 8 amewashukuru wote abao walisimama nap baada ya kumpoteza mtoto wake.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alipakia video akiwa na familia yake na kuandika ujumbe wa shukrani.

"ASanteni kwa kila mmoja kwa maombi yenu na shukrani kwa Mungukwa maisha na nguvu, asanteni nyote kwa kusimama na mimi pamoja na familia yangu

Mungu awabariki nyote, Mungu atukuzwe," Size 8 Aliandika.

Bali na kumpoteza mtoto wake msanii huyo alimshukuru Mungu kwa kipaji cha uhai, baada ya kufanyiwa upasuaji.

Size 8 na mumewe DJ Mo walitangaza habari za ujauzito, mwezi wa Agosti.

Kupitia kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii ya instagram waliwafahamisha mashabiki wao kwamba mtoto wao ameaga dunia.

"Tuna mipango, Lakini Mungu ana mipango bora zaidi… kama vile umeona kwenye YouTube, Ndio ilitokea, Mungu anakupea na anachukua

Imekuwa karibu miezi 5 akipambana na Joto ambalo lilipiga 213, operesheni ya dharura

Asante Dk NYAMU na timu @komarockmodern kwa kumwokoa mke wangu, .. kasi ambayo ulifanya yote haya - kwa kweli nitakumbuka siku zote uliokoa mke wangu na kuhakikisha yuko salama…

Asante Mungu, unabaki kuwa Mungu katika hali zote. mtoto hakuweza kuwa hai, lakini mke wangu yuko hai na salama. @ size8 niko na wewe - hadi mwisho," DJ Mo aliandika.