Juakali amsherehekea mkewe kwa ujumbe maalum anapoadhimisha siku ya kuzaliwa

Muhtasari

•Baba huyo wa watoto watatu  amemtaja mkewe kama mwangaza wa familia na mama mzuri wa watoto wao.

•Juakali amesema kuwa mkewe ambaye ni mtangazaji amemsaidia sana katika taaluma yake ya usanii na kumtakia maisha marefu zaid

Image: INSTAGRAM// LILY ASIGO

Bi Lily Asigo ambaye ni mke wa mwanamuziki Paul Julius Nunda almaarufu kama Juliani anasherehekea siku yake ya kuzaliwa hivi leo, Oktoba 11.

Juakali amechukua fursa  hiyo kumshukuru mkewe kwa majukumu makubwa ambayo anatekeleza katika familia yao.

Baba huyo wa watoto watatu  amemtaja mkewe kama mwangaza wa familia na mama mzuri wa watoto wao.

'Watu wangu nisaidieni kumtakia mke wangu mzuri kheri za kuzaliwa. Asante kwa kuwa wewe. Asante kwa kuwa mwangaza wa familia. Asante kwa maombi. Asante kwa kutuwakilisha vizuri hadharani. Asante kwa kuwa mama mzuri kwa watoto wetu" Juakali alimwandikia Bi. Asigo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Juakali amesema kuwa mkewe ambaye ni mtangazaji amemsaidia sana katika taaluma yake ya usanii na kumtakia maisha marefu zaidi.

"Asante kwa nguvu unayonipa kuendelea kukazana kwenye sekta hii ngumu. Shukran kwa kunipondoa kwenye video zangu he he he. Nakusherehekea sana kwa kufuata ndoto zako na nitaendelea kukuunga mkono asilimia mia kwa mia.

Hii ni siku maalum sana kwako. Nakutakia maisha marefu, furahia kabisa. Tunakupenda, kheri za kuzaliwa" Alisema Jua Kali.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa kwa zaidi ya miaka nane na wameendelea kushiliana katika taaluma zao za usanii.