Umeingiwa na kiburi juu ya netflix,'Eric Omondi amsuta Eddie Butita baada ya kumlipisha milioni 3.5 ili kuelekeza shoo yake

Muhtasari
  • Shoo yake mchekeshaji Eric Omondi ya Wife material inatarajiwa kurejea kwenye runinga zetu hivi karibuni

Shoo yake mchekeshaji Eric Omondi ya Wife material inatarajiwa kurejea kwenye runinga zetu hivi karibuni.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Omondi amefichua kwamba ana shida ya mwelekezi wa kipindi hicho, huku akimuomba mchekesheji Butita kuelekeza shoo yake.

Butita alimsihi Omondi azungumze na meneja yake, na kumwambia kwamba kuelekeza shoo hiyo ni milioni 3.5.

Kulinagana na Eric Butita amekuwa rafiki yake wa karibu na hajakuwa akipokea simu zake.

Pia alimshtumu Butita na kusema kwamba ameingiwa na kiburi baada ya kuandikwa na Netflix.

Aidha Eric aliweka wazi hana shida ya pesa kwani hata yuko taari kulipa zaidi ya pesa anazohitaji.

"Hii ni tatizo na sekta yetu ya burudani @ddiebutita si tu rafiki yangu mzuri sana lakini ninamfikiria kama ndugu yangu

Lakini Sasa Akianza Kusema Ati mimi  napaswa kuzungumza na timu yake na Achukui Simu Zangu

Kwa nini ungenipeleka kwa meneja wako na bado tunaweza kuzungumza na kufanya biashara😥😥🤦♂️🤦♂️🤦♂️ ... Sisi Hatuna Shida ya Pesa Tunakuita tu kutoa huduma zako za kitaaluma AMA JUU ya Netflix Sasa Umeingiwa na kiburi😥😥shika simu zangu shoo itaanza wiki ijayo Jumanne na tunakuhitaji. Umeomba dola 35,000 ambazo ni karibu milioni 3.5 na tuko tayari kulipa hata zaidi. @eddiebutita," Eric Alsema.