King Kaka angetapika kwa harufu ya chakula - Nana Owiti asimulia

Muhtasari

•Bi Owiti amesema kuwa walipambana sana na mwanamuziki huyo ili akubali kula kwani hakuwa anataka.

•Owiti ameelza kwamba alikuwa anasaidiana na mama mkwe kumshawishi bwanake akule chakula na ilikuwa inamchukua muda mrefu kumaliza kula chakula kidogo.

Image: INSTAGRAM// KING KAKA

Mtangazaji Nana Owiti ambaye ni mke wa mwanamuziki mashuhuri Kennedy Ombima almaarufu kama King Kaka amefichua kuwa haikuwa rahisi kwa mumewe kuweza kula tena wakati alikuwa anaugua.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bi Owiti ameeleza kuwa  walimpatia Kaka chakula laini tu katika siku za kwanza alipoanza kurejesha uwezo wa kula.

Bi Owiti amesema kuwa walipambana sana na mwanamuziki huyo ili akubali kula kwani hakuwa anataka.

"Hii ilikuwa siku yake ya kwanza kula chakula kisicho maji maji. Tulianza kwa kumpatia chakula laini kwanu harufu tu ya cgakula haswa kile cha hospitali ingefanya aanze kutapika. Yaweza kuonekana kama ilikuwa rahisi lakini tulipambana sana ili akubali kula" Bi Owiti alieleza chini  ya video iliyoonyesha King Kaka akiwa anang'ang'ana kula chakula.

Owiti ameeleza kwamba alikuwa anasaidiana na mama mkwe kumshawishi mumewe akule chakula na ilikuwa inamchukua muda mrefu kumaliza kula chakula kidogo.

Hata hivyo alieleza kuwa hatua yake ya kuanza  kula ilikuwa ushindi mkubwa.

"Ilifikia wakati mimi na mama yake tulionekana kama maadui kwani tulikuwa tunamlazimisha akule. Kwa hivyo wakati ambapo chakula kililetwa na tujaribu kusema 'tafadhali kula' ilikuwa kesi. Huu ulikuwa ushindi mkubwa .  Alikuwa karibu kumaliza chakula hicho kidogo na saa moja" Alieleza Nana.

Wiki chache zilizopita mwanamuziki huyo alitangaza kuwa  afueni yake ilikuwa imeanza kurejea huku akieleza kuwa daktari wake alikuwa amempatia maelezo maalum kuhusiana na lishe.

"Acha nikunywe chai.. saa hii nakula manduma kila baada ya masaa matatu. Nimekuwa nikifuatia maagizo ya daktari kuhusu lishe lakini nitarejea. Lazima tudrop EP, lazima tutoe mangoma" King Kaka alisema kupitia mtandao wa Instagram.

Ingawa Kaka amepiga hatua kiasi katika safari yake ya kupata afueni kikamilifu, mkewe ameeleza kuwa bado hisia yake ya ladha haijarejea kikamilifu.

Msanii huyo anasherehekea kwamba ameweza kuondoka hospitalini tayari na kueleza kuwa atajitahidi kurejesha uzito wa mwili ambao alipoteza baadae.