'Nimejifunza kumheshimu,'Mtangazaji Massawe afunguka kuhusu kuwa mzazi wa mtoto kijana

Muhtasari
  • Mtangazaji Massawe afunguka kuhusu kuwa mzazi wa mtoto kijana
Image: Instagram/Massawe

Mtangazaji anayesherehekewa sana nchini wa Radiojambo Masswe Japanni, kwa mara ya kwanza kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alishiriki, mambo kadha wa kadha kuhusu kumlea mtoto wake Imani.

Imani yuko katika umri wa ujana, ambapo vijana wengi hutaka kukaa peke yao kwa muda mwingi.

Kupitia kwa video aliyopakia kwenye ukurasa wake, Massawe na mwanawe walishiriki jinsi wamekuwa huku mwanawe Massawe akimuuliza ashiriki uzoefu alio nao kwa kuwalea.

Massawe alijibu na kusema;

"Kazi kazi kazi tupu."

Mtangazaji huyo aliendela na kueleza jinsi hakuelewa kwa nini mwanawe alitaka muda wake peke yake.

"Wewe na nafasi yako, huwa nashinda kumuita  Imani ashuke, Imani tafadhali tunaweza kutumia wakati pamoja. Vijana wanaweza kukusukuma juu ya ukuta. Lakini nimejifunza kumheshimu na kuheshimu nafasi yake, lakini imekuwa safari nzuri, "alielezea.

Mwanawe Massawe alipinga na kumwambia kwamba hajakuwa akimpa nafasi ya kuwa peke yake licha yake kutaka nafasi hiyo.

"Imani utakuwa na muda wa kukaa peke yako, wakati huu nakuhitaji kila wakati, kila mtoto ana tabia,utu wake wazazi hawapaswi kulinganisha watoto wao

Kama wewe ni mazazi lea watoto wako vile unaweza hakuna mwongozo,husijihisi vibaya kwa maana kuna mama mahali anajihisi kuwa bora, wewe ni mama bora usikubali mtu akuzushe," Alizungumza Massawe.

Huku mwanawe akizungumza mafunzo ambayo amepokea kutoka kwa mama yake alikuwa na haya ya kusema;

"Kile mama yangu amenifunza ni kuwa nijitegemee na cha muhimu ziadi ni muogope Mungu," Imani alisema.