Umenipenda sawa, nataka kuwa mzee nawe-Ujumbe wa Diana kwa mumewe Bahati

Muhtasari
  • Diana alimshukuru mumewe kwa kuwa naye na kumpenda na kukiri kwamba anataka kuzeeka naye milele
Image: INSTAGRAM//DIANA MARUA

Licha ya changamoto na kejeli ambazo hupokea kutoka kwa mashabiki, Diana Marua na mummewe Bahati bila shaka ni wanandoa wa kupigiwa mfano na wengi.

Diana Marua kuitia kwenye ukurasa wake wa instagram amepakia picha ya zamani akiwa na mumewe Bahati yaani TBT na kuandika ujumbe huku akimsifu mumewe.

Diana alimshukuru mumewe kwa kuwa naye na kumpenda na kukiri kwamba anataka kuzeeka naye milele.

"Nimepata tu arifu kutoka kwa simu yangu ... Tazama Kumbukumbu Zako Miaka 5 Iliyopita, LEO 🙆

Jamani Mwenzangu wa Maombi @BahatiKenya 😝 umenipenda sawa. Ninaangaza TOFAUTI! Nataka kuzeeka na wewe MFALME WANGU ❤️👑❤️ #TBT 🤣

usimchezee au kumtania MUNGU 🥳," Aliandika Diana.

Ni picha mabayo ilivutia mashabiki wake na walikuwa na haya ya kusema;

terencecreative: Kabla ya Kemikal 😂😂😂😂

cherowinnie: Aki pesa wewe. Find me❤️❤️

jennie_george_: Kumbe ni pesa sina ...sura Niko nayo😂

daphney_amisi: MMETOKA MBALI😍😍😂WE CAN'T JOKE WITH GOD ❤️

shikoshixxs: Aki pesa wewe nikikupata unifanye kama diana