'Ikiisha kila mtu apambane na premium tears yake,'Akothee asema hataficha uhusiano wake na mpenzi wake

Muhtasari
  • Akothee asema hataficha uhusiano wake na mpenzi wake
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mjasirimali na msanii Akothee ameonyesha kwamba uhusiano wake na mpenzi wake Nelly Oaksni wa kupigiwa mfano na wengi.

Akothee pia amewashauri mashabiki wake wamuombee wabarikiwe na mtoto hivi karibuni.

Kupitia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii Akothee amethibitisha kwamba mapenzi yao yanaendelea kunoga kila kuchao.

"Hamna kitu tamu kama kuchumbia mtu ambaye huwezi ficha, mchezo huo ni wa kijinga

Unacheza nani moyo wako?Mimi huwezi Nificha kama pin ya mpesa .kama tunapendana 🤣🤣🤣, oooh sore If I am in love we are . Ikiisha kila mtu apambane na premium tears yake

Kwa SAA huu tunapendana kwa hivyo tuunge mkono na uungane nasi na uombe nasi tubarikiwe na mtoto hivi katibuni💋💋💋Kemikali imeingia 🤣🤣," Aliandika Akothee.

Ni wazi kuwa uhusiano wake Akothee na Nelly umekuwa ukipokea kejeli kutoka kwa mashabiki, lakini licha ya hayo yote mapenzi yao yananoga.