Ninalaani aina zote za vurugu bila kujali ni nani anayehusika,'Janet Mbugua azungumza baada ya mumewe kudaiwa kumpiga mwanamke

Muhtasari
  • Janet Mbugua azungumza baada ya mumewe kudaiwa kupiga mwanamke
Janet Mbugua
Image: Hisani

Janet Mbugua kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter amelaani vikali aina yeyote ya vurugu, kulingana naye hatojali nani aliyehusika.

Ujumbe wake ni kama vile ufuatao;

"Nimesikitishwa na kuongezeka kwa visa vya Ukatili wa Kijinsia. Katika muongo mmoja uliopita, nimejiunga na sauti yangu kwa juhudi za #EndGBV

Ninalaani aina zote za vurugu bila kujali ni nani anayehusika na ataendelea kusema dhidi yake. Tuna sheria nchini Kenya na haki inapaswa kutawala," Janet Ameandika.

Usemi wake unajisiri saa chache baada ya mwanamke, mmoja kudai kwamba mumewe Janet na ndugu yake waliwataishia maisha wakiwa na dada yake.

Ni video ambayo imeenea sana mitandaoni huku ikiibua mdahalo mkali.

“Jana dada yangu na mimi tulishambuliwa na mapacha wa Ndichu kwa kuwakataa kwa heshima. Walitishia kutupiga risasi na kuharibu maisha yetu

Dada yangu alinyongwa na Paul Ndichu wakati mpenzi wake aliyemjia alikuwa akinyongwa na Eddie."

Katika ujumbe wake, mwathiriwa alisema tukio hilo limemwacha akiwa na hofu.

Kwenye video iliyoshirikiwa na Boniface Mwangi, mtu mmoja anaonekana akiharibu gari lililokuwa limeegeshwa nje ya hoteli.

Kulingana na ripoti ya wanawake hao, wanadai wanaume wawili ni Paul Ndichu na ndugu yake Eddie Ndichu, na mwingine ni mpenzi wa dada yake.