Ni ngumu sana kumtazama mwanamume akimshambulia mwanamke-Tedd Josiah

Muhtasari
  • Wanamitandao,watu mashuhuri,wasanii, wananchi wameungana pamoja na kulaani vurugu na unyanyasaji wa kijinsia, ambao unaenea kila kuchao
tedd josiah
tedd josiah

Wanamitandao,watu mashuhuri,wasanii, wananchi wameungana pamoja na kulaani vurugu na unyanyasaji wa kijinsia, ambao unaenea kila kuchao.

Sio nyumbani tu bali vurugu vyovyote ambavyo vina mwathiri mwanamke.

Haya yanajiri baaada ya Mumewe Janet Mbugua na pacha wake Paul Ndichu na Edddie Ndichu kudaiwa kuwapiga wanawake mwishoni mwa wiki.

Tumeshuhudia,kuona, na kuskia jinsi watu wengi wamepoteza maisha yao kutokana na unyanyasaji wa familia.

Pia haya yanajiri baada ya mwanaraiadaha Agnes Tirop kudaiwa kuuwawa na mpenzi wake.

Mzallishaji Tedd Josiah kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, amesema kwamba ni jambo ngumu sana kuona mwanamume akimpiga mwanamke kwa sababu anaweza.

"Ni ngumu sana kumtazama mwanamume akimshambulia mwanamke KWANI ANAWEZA. Ni ngumu sana kusikia mwanaume akimtukana mwanamke kwa sababu anaweza," Aliandika Tedd Josiah.

Hata hivyo amesema kwamba nguvu na ukubwa ambao mwanamume amepewa na Mungu ni wa kumlinda mwanamke na wala sio kumdhuru.

"Ukubwa waliopewa wanaume na Mungu haukukusudiwa kuwadhuru wanawake wao bali kuwa walinzi wa wanawake

Ukatili wa kijinsia sio suala ambalo tunapaswa hata kufanya kampeni dhidi yake. Kwa sababu kwa sasa wabunge wetu wangepaswa kuunda sheria ngumu ya kutosha kuwafanya watu wenye jeuri wafikirie mara 10 kabla ya kuinua mikono yao kwa mwanamke mwingine, mtoto au mwanamume

Ninawasihi wanaume zaidi WAZUNGUMZE na kuwaita marafiki wao ambao wanaweza kushiriki katika UWAKI nje. Tunaweza kukomesha hii 🛑."