Mke wangu aliniambukiza virusi vya ukimwi na kuniachia watoto 2-Jamaa asimulia

Muhtasari
  • Jamaa asimulia jinsi aliambukizwa ukimwi na mkewe
sad man
sad man

Asilimia kubwa ya wanawake, husema kwamba waume wao ndio waliwaambukiza virusi vya ukimwi, kwa kuenda nje ya ndoa.

Kama ndoa haina uaminifu ndani yake, hamna haja ya kukaa katika ndoa kama hiyo kwani utapatwa na madhara mengi.

Ni muhimu sana kila mwanandoa kuwa na uaminifu kwa mwenzake, na kujali kuhusu ya mwenzake.

Nikiwa kwenye ziara yangu, nilipatana na jamaa aliyefahamika kama Timothy, ambaye alinisimulia machungu ya ndoa yake.

Kulingana na Timothy, mkewe alimuambukiza virusi vya ukimwi lcha yake kufahamu ana virusi miaka 10 iliyopita.

Hii hapa hadithi yake;

"Nilipomuona mke wangu kwa mara ya kwanza, nilijua na kufahamu kwamba  atakuwa mke mwema, na ni mwanamke ambaye namuhitaji katika maisha yangu

Alikuwa amevaia tu ngozi ya kondoo, kwani alikuwa na mipango ya kando na wala sio mmoja, alipata virusi vya ukimwi, na kuniambukiza

Baada yangu kugundua, aliniachia watoto wawili, na kuniambia kwamba sio mimi tu pekee ameniambukiza virusi hivyo."

Baada ya janga la corona kuripotiwa nchini mwaka jana, wengi wa vijana na sio vijana ata wanandoa, wamesahau kuwa kuna virusi vya ukimwi na kulegeza kamba kupigana na virusi hivyo.

Haya basi tujihadhari na virusi vya ukimwi pia, tunapopigana na virusi vya corona.