Mume wangu anawakera nini,sijawahi enda kwa mganga-Nyota Ndogo

Muhtasari
  • Nyota Ndogo ni miongoni mwa wasanii wa kenya ambao wameinuka kila siku kwa ajili ya bidii yao
Image: INSTAGRAM// NYOTA NDOGO

Kwa muda sasa msanii kutoka mkoa wa pwani, Nyota Ndogo amekuwa akitupilia mbali uvumi kuwa amekuwa akitumia uchawi, kwenye biashara yake.

Nyota Ndogo ni miongoni mwa wasanii wa kenya ambao wameinuka kila siku kwa ajili ya bidii yao.

Kulingana na Nyota Mungu humpa mtu mwenye bidii,na kile anachoogopa maishani kwake ni shida.

"Jamani MUNGU umpa mwenye bidii. Roho yako kama ni nzuri ama ni mbaya binadamu hawezi kujua lakini uwezi kufake mbele ya MUNGU

mimi jamani mimi naogopa shida Sana maana naijua na ndio maana Sina time ya kulala mpaka saa mbili.

Binadamu utaka mtu ateseke wakuseme wakucheke wakuache upate tabu. Huyu ni maid kama nilivyokua mimi kitambo but amekataa Kua mimi nilikua maid na Leo nipo hapa yani mpaka @nyotandogo_jikoni naambiwa naiendea kwa nganga ndio nipate wateja jamani

Hivi HAMUAMINI KUA MUNGU YUPO NA ANASIKIA MAOMBI?. alafu mume wangu anawakerea nini? Post ya hotel yangu Jana inausikana vipi na mume wangu?

Ama mulifikiria niliachwa kweli na mukasherekea mume alipokuja kwa mke wake mkapandwa na hasira?."

Aidha msanii huyo alikanusha madai kwamba amekuwa akienda kwa mganga, na siku ambayo atakanyaga kwa mganga ndio utakuwa mwisho wake.

" SIJAWAI KWENDA KWA MGANGA SIJAWAI FIKIRIA HATA KWENDA KWA MGANGA NA NAAMINI SIKU NITAKWENDA KWA MGANGA NDIO MIMI ITAKUA MWISHO WANGU. KITU AMUJUI NI KUA MIMI NIMTU WA KUOMBA MUNGU SANA.

KAZI YA KUMUENDELEA BINADAMU MWENZANGU ETI MGANGA ANITIBU NIKAMA NIMEONA MUNGU HANA NGUVU

IMANI YANGU IPO JUU SANA KWA MUNGU. NA KILA NIKIOMBALO NAKIOMBA KWA MOYO ANANIPA MAANA NIPO CLEAN.

UKINIFATA KWA USHAURI NAWEZA KUKUJENGA UKINICHUKIA UNAPOTEZA MUDA. PIA UWA NAPATA INBOX NYINGI WATU WANATAKA NIWAPELEKE KWA MGANGA ALINIRUDISHIA MUME WANGU NA WAO WARUDISHE WAO. POLENI SIJUI MGANGA YOYOTE," Alisema Nyota.

Msanii huyo alivuma sana baada ya kuachwa na mumewe siku ya 'Fools day' mwaka huu.