Mke wangu amekataa kutoa sindano ya 'family planning' ili tupate watoto-Mwanamume alia

Muhtasari
  • Furaha ya ndoa ni kuwa mtoto, au watoto, ili familia izidi kukua na kuongezeka kila kuchao
  • Katika karne ya sasa wanandoa wengi wanatumia dawa za upangaji uzazi, wa aina tofauti ili kuzuia kupata ujauzito amba hujapangwa
  • Jamaa aeleza vile mkewe amekuwa akitumia dawa za upangaji uzazi ili asipate mtoto naye
sad man
sad man

Furaha ya ndoa ni kuwa mtoto, au watoto, ili familia izidi kukua na kuongezeka kila kuchao.

Katika karne ya sasa wanandoa wengi wanatumia dawa za upangaji uzazi, wa aina tofauti ili kuzuia kupata ujauzito amba hujapangwa.

Sio wanandoa tu bali kuna baadhi ya vijana na hata watoto wa shule baada ya kufanya ngono wanatumia dawa za kuzuia mimba bila ya kujua madhara yake katika maisha za usoni.

Wanaume wengi wamekiri kupata watoto nje ya ndoa baada ya wake zao kukataa kupata ujauzito kwa kutumia dawa za kupaga uzazi.

Mwanamume mmoja alisimua jinsi amekuwa akitarajia kupata mtoto na mke wake bila mafanikio.

Lakini sababu ya kuto fanikiwa ni ipi?Huu hapa usimulizi wake;

"Nimekuwa kwa ndoa na mke wangu kwa takriban mwaka mmoja sasa, anatumia family planning nimemsihi kwa miezi sasa atoe sindano hiyo ili tupate mtoto lakini hataki

Mke wangu amekuwa akisema kwamba lazima tujipange, kwani ana watoto wawili abao nilimuoa nao, sijuia anataka tujipange hadi lini na sababu ya kytotaka iwe na mtto naye, licha yangu kumpenda na maisha yanu yote," Alisimulia Jamaa huyo.