Watu mashuhuri waliobarikiwa na vifungua mimba mwaka wa 2021

Muhtasari
  • Ni matamanio na furaha ya kila wanandoa, au wanawae kubarikiwa na watoto wenye afya, baada ya safari ndefu ya ujauzito
Image: INSTAGRAM// MULAMWAH

Ni matamanio na furaha ya kila wanandoa, au wanawae kubarikiwa na watoto wenye afya, baada ya safari ndefu ya ujauzito.

Mwaka wa 2021, tumeona na kushuhudia baadhi ya watu mashuhuri ambao wamebarikiwa na vifungua mimba wao.

Hii hapa baadhi ya orodha ya watu waliobarikiwa na watoto wa kwanza mwaka wa 2021;

1.Vera Sidika na Brown Mauzo

Mwanasosholaiti Vera na mumewe Mauzo, walibarikiwa na kifungua mimba wao tarehe 20/10, huku wakifichua kwamba msichana wao alizaliwa saa nne na dakika 21 asubuhi.

2,Vanessa Mdee na Rotimi

Msanii Rotimi na Vanessa walipatana kwa sherehe ambapo wallijuana na baada ya muda kuanzisha uhusiano wao.

Wawili hao walibarikiwa na mtoto wao wa kwanza Septemba 29.

3.Mulamwah na Soni

Mchekeshaji huyo na mpenzi wake wamekuwa pamoja kwa muda sasa, na ni wapenzi wa kupigiwa mfano mwema na wengi.

Mwaka huu walibarikiwa na kifungua mimba wao Septemba 20.

Miongoni mwa watu wengine ni pamoja na Willis Raburu na Ivy Nyamu, mwanablogu Xtian Dela na mpenzi wake.